Showing posts with label KIMATAIFA. Show all posts
Showing posts with label KIMATAIFA. Show all posts

Tuesday, June 3, 2014

Hii sasa kali…cheki picha mpya za Rihanna zinazoleta gumzo kwenye internet.

 

1
Rihanna amewahi kuacha gumzo mara nyingi kutokana na picha zake zinazosambaa mtandaoni. Mara nyingine tena picha za Rihanna ndio zinakuwa picha zinazoangaliwa sana hivi sasa kwenye mtandao.
Picha hizi amepiga akiwa kwenye red carpet ya CFDA Fashion Awards huko New York.
2
3
4
Capture



src
AyoTZ

Sunday, June 1, 2014

Kwa hiyo Wachina wamekuja na hii sio ?!!


BEGI1

Unaambiwa Wachina wameamua kuonyesha maajabu mengine kwa kufanya begi kuwa baiskeli tena ikiwa na uwezo wa kubeba mtu mmoja na ikiwa ni baiskeli yenye ufanyaji kazi kama wa pikipiki.
BEG2

Sanduku hili ambalo lina matairi mawili lina uwezo wa kwenda umbali wa Kilomita zisizopungua 60 kwa kasi ya Kilomita 20 kwa saa na linatumia nishati ya umeme ambayo ni betri.
Baiskeli hii imezinduliwa na mkulima aitwae He Liang ambae ametumia miaka 10 kulitengeneza sanduku hili ambalo lina nafasi ya kutosha ya kuweka nguo ambapo likiwa tupu unaambiwa lina uzito wa Kilo 7

src
AyoTz

Sunday, March 30, 2014

Viongozi wa nchi za Maziwa Makuu wawekea vikwazo viongozi wa waasi DRC


Mkutano wa viongozi wa mataifa ya Kanda ya Maziwa Makuu mjini Luanda Angola
Mkutano wa viongozi wa mataifa ya Kanda ya Maziwa Makuu mjini Luanda Angola

Kwa mara ya kwanza marais wa nchi za Kanda ya Maziwa Makuu, ICGLR wamependekeza kuweko na vikwazo vya kisiasa na kiuchumi dhidi ya makundi ya wapiganaji yanayopatikana mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Kwenye mkutano wa siku moja mjini Luanda siku ya Jumatano viongozi hao Marais  Edourdo dos Santos wa Angola, Dennis Sasou Nguesso wa Kongo Brazzaville,Yoweri Museveni wa Uganda, Joseph Kabila wa Kongo, na Paul Kagame wa Rwanda pamoja na Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma, aliyealikwa kuhudhuria, wameomba pia kurejeshwa haraka Kongo wapiganaji wa zamani wa kundi la M23 walioko Uganda na Rwanda.

Kwenye taarifa yao ya pamoja, marais sita wa nchi za Maziwa Makuu pamoja na Afrika ya kusini wamependekeza kuweko na mtizamo wa pamoja kwa ajili ya kupambana na makundi yote ya wapiganaji yalioko mashariki mwa DRC.

Ma rais hao wamepenekeza kuwawekea  vikwazo vya kisiasa na kiuchumi  viongozi wa makundi hayo ya wapiganaji.

Kukuza  uhusiano na ushirikiano wa kikanda na kimataifa  katika kufahamu mahala waliko viongozi wa makundi hayo ya wapiganaji  ambayo bado ni tishio kwa usalama wa nchi za ICGLR.

Kuhusu hali ya usalama mashariki mwa DRC, rais Joseph Kabila aliwapa maaelezo marais wenzake kuhusu harakati za kijeshi zinanzoendeshwa na jeshi la Kongo dhidi ya waasi wa ADF kutoka Uganda. Na katika taarifa  yao ya pamoja, marais wamepongeza mafanikio ya operesheni hizo na namna zinaendeshwa kwa ushirikiano na kikosi cha kikanda.

Mkutano huo wa marais ulizungumzia pia tatizo la kidiplomasia lililoko hivi sasa baina ya Rwanda na Afrika ya Kusini. Ilikua mara ya kwanza kwa marais Paul Kagame na Jacob Zuma kukutana tangu uhusiano baina ya nchi zao mbili kuzorota kufuatia hatua za kuwaondoa wanadiplomasia wao.

Rais Zuma aamewambia wandishi habari baada ya mazungumzo kwamba yeye na mwenzie wa Rwanda wamekubaliana kufanya mazungumzo ya moja kwa moja ilikumaliza ugomvi kati yao.

Umoja wa mataifa pia unaelezea kufurahishwa na operesheni za kijeshi dhidi ya waasi wa ADF,Kwenye mkutano na wandishi habari siku ya Jumatano mjini Kinshasa, msemaji wa kijeshi wa kikosi cha Umoja wa Mataifa,MONUSCO Lt kanali Felix Basse, amesema kwamba jeshi la Kongo limethibiti maeneo muhimu yaliokaliwa na waasi hao kwa zaidi ya miaka 6. 

src
VOA

Nchi tatu Afrika zaanza juhudi za nishati ya nuklia

Ramani inayoonesha nchi tatu barani Afrika zenye juhudi ya kuongeza nishati ya nuklia
Ramani inayoonesha nchi tatu barani Afrika zenye juhudi ya kuongeza nishati ya nuklia
                                      
Nchi tatu barani Afrika zimeanza juhudi za kuongeza nishati ya nuklia katika mikonga yao ya umeme. Kenya na Nigeria zinataka kuanza nishati ya nuklia wakati Afrika kusini – nchi pekee kusini mwa bara la Afrika ambayo ina mitambo ya nuklia – inataka kupanua uwezo wake. Mpaka sasa, mataifa ya Afrika yamekuwa yakitegemea mifumo ya kizamani kuzalisha umeme – nguvu za maji au mkaa wa mawe. Lakini vyanzo hivyo vimekuwa na madhara ya kijamii na mazingira, na hata kusababisha watu kuhama makazi yao. Lakini swali kubwa linaloulizwa ni jee Afrika ina uwezo wa kuanza nishati ya nuklia?

Kulingana na takwimu za Benki ya Dunia ni chini ya asilimia 10 tu ya jumla ya makazi yote ya watu barani Afrika ambayo yanapata umeme. Hali hiyo kwa namna kubwa inaathiri pia maendeleo ya viwanda na sekta nyinginezo katika bara masikini kuliko yote duniani.

Shida hiyo ya umeme ndio inasababisha baadhi ya nchi za Afrika kutafakari nishati ya nuklia – mfumo ambao unatumiwa katika baadhi ya nchi zinazoendelea na zilizoendelea kama vile Marekani, India na China.

Kelvin Kemm, mtaalam wa fizikia ya nuklia huko Afrika Kusini, anasema Afrika inahitaji kuangalia nje ya mifumo ya uzalishaji umeme inayotumika sasa. Anasema “kwa jumla inapata umeme unaotokana na nguvu ya maji, na kila mtu anajua kuwa ukame wa miaka kadha barani humo unawezekana. Kwa hiyo ni hatari kujenga uchumi kwa kutegemea umeme unaotokana na maji.”
Matumizi ya nishati ya nuklia nchini Afrika kusiniMatumizi ya nishati ya nuklia nchini Afrika kusini
x
Matumizi ya nishati ya nuklia nchini Afrika kusini
Matumizi ya nishati ya nuklia nchini Afrika kusini


Afrika Kusini ni nchi pekee barani humo ambayo ilifanikiwa kutengeneza teknolojia ya nuklia, na iliwacha mpango wake wa silaha za nuklia katika miaka ya 90. Leo hii mtambo wa nuklia wa Koeberg unatoa karibu asilimia tano ya umeme wa nchi hiyo. Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma anasema anataka kuongeza uwezo wa umeme wa nuklia ili kupunguza kutegemea umeme unaotokana na mkaa wa mawe.

Kenya na Nigeria zinasema nazo zinaandaa mipango yao ya nuklia kukabiliana na ongezeko la mahitaji ya umeme kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu. Mtaalam Kelvin Kemm anasema mahitaji ya umeme Afrika ni makubwa sana kiasi kwamba mifumo ya sasa ya uzalishaji umeme haiwezi kukidhi mahitaji hayo kama vile ambavyo nuklia ingeweza.

Wapinzani wa nishati ya nuklia wanasema teknolojia hiyo ina hatari zake, wakikumbusha ajali zilizotokea Fukushima, Japan au Chernobyl katika Soviet Union ya zamani. Lakini hata wapinzani hao wanahofu kwamba hatari hizo huenda zikafunikwa na ukweli kwamba mahitaji ya umeme ni makubwa mno.

Wataalam wanasema itachukua miaka, hata miongo kadha, kabla Afrika kupata namna ya kukidhi mahitaji ya umeme, ama kwa nishati ya nuklia au njia nyinginezo. Lakini kila mtu anakubali kuwa umeme zaidi unahitajika kuleta mwanga barani Afrika
 
src
VOA

Saturday, March 22, 2014

UN yaripoti uovu Sudan Kusini

 

Umoja wa Mataifa umesema mapigano yenye sura ya kikabila yaliyozuka katikati ya Desemba mwaka jana Sudan Kusini yamesababisha mauaji ya kikatili na unyanyasaji dhidi ya maelfu ya raia na kampeni ya kukashifu umoja huo.
Südsudan Flüchtlinge Polizei 07.01.2014 Wakimbizi na Polisi nchini Sudan Kusini
Mkuu wa shughuli za kusimamia amani wa Umoja wa Mataifa Herve Ladsous ameliambia baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa pamoja na makubaliano ya kusitisha mapigano ya Januari 23, lakini jeshi tiifu kwa rais Salva Kiir na wapiganaji waasi wanaoongozwa na makamo wa rais wa zamani alieondolewa madarakani Riek Machar wameendelea na harakati zao za kijeshi na kuyapa kisogo mazungumzo muhimu ya kisiasa kwa lengo la kupatikana suluhisho la mgogoro huo.
Kuzuka mapigano
Südsudan Rebellen 10.02.2014 Wapiganaji waasi katika baadhi ya miji
Mapigano Sudan Kusini yalizuka Desemba 15 miongoni mwa kikosi cha jeshi cha ulinzi wa rais mjini Juba, ambapo kwa kasi yakasambaa katika maeneo tofauti ya nchi hiyo na kuchukua sura ya mwelekeo wa mapigano ya kikabila kati ya kabila la Dinka, lenye kumuunga mkono rais Kiir na Nuer lenye utiii kwa Machar.
Afisa huyo mwandamizi wa Umoja wa Mataifa, Ladsous amesema mgawiko wa kisiasa umesababisha mgogoro kwa hivi sasa kwa kuathiri maisha ya kila mtu mmoja mmoja pamoja na utendaji wa serikali ya Sudan Kusini na taifa lenyewe kwa ujumla. Amesema ripoti ya uchunguzi ya awali inaonesha mauwaji pamoja na ukiukwaji mbaya sana haki za binaadamu umetekelezwa na pande zote zinazohasimiana katika mgogoro huo.
Onyo la kuendelea mapigano
Konflikt im Südsudan Flüchtlinge 17.01.2014 Wakimbizi wakihangaikia maji safi
Aidha afisa huyo ameonya kwamba kuendelea kwa muda mrefu kwa mapigano hayo kunaweza kutoa nafasi ya majeshi ya kikanda kuingia zaidi katika taifa hilo. Ladsous vilevile ameonya kuwa hakutakuwa na hatua yoyote ya maana itakayofikiwa na mataifa yalio katika Jumuiya ya maendeleo mashariki na pembe ya Afrika- IGAD katika utatuzi wa mgogoro huo mpaka hitaji muhimu la upinzani la kutaka kuachiwa huru kwa wafungwa wanne walisalia gerezani litekelezwe. Watuhumiwa hao walipandishwa kizimbani Machi 11 kwa tuhuma za uhaini.
Ladsous amelitaka baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kulaani kampeni yeyote dhidi ya operesheni ya ulinzi wa amani nchini Sudan Kusini ambao inatoa hifadhi kwa wakimbizi 75,000 kati ya watu 800,000 waliopoteza makazi yao kutokana na vurugu hizo. Na amemtaka rais Kiir kulaani na kuwalekeza maafisa wa serikali na chama chake kiachana na vitendo hivyo mara moja. Amesema vitendo hivyo dhidi ya ujumbe wa kusimamia amani Sudan kusini , vinaweza pia kuhatarisha maisha ya watoa huduma.
Baadae akizungumza na waandishi wa habari balozi wa Luxembourg katika Umoja wa Mataifa Sylive Lucas hali hiyo haikubaliki na amekubali kutuma ujumbe mkali nchini Sudan Kusini. Aidha Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amependekeza kwa baraza hilo la usalama kuongzea uwezo UNMIS katika kiwango kilichokubaliwa Desemba mwaka jana kufikia wanajeshi 12,500, shabaha ikiwa kuwalinda raia, kufanikisha kufikisha misaada ya kiutu na kuchunga vitendo vya ukiukaji wa haki za binaadamu.
Mwandishi: Sudi Mnette APE
Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman

CHINA YASEMA IMEONA KITU KATIKA BAHARI YA HINDI KINACHODHANI NI MABAKI YA NDEGE ILIYOPOTEA YA MALAYSIA

                
Picha iliyotolewa na vyombo vya habari vya China vikionyesha kitu kipya kilichogunduliwa na satellite za nchi hiyo kikielea katika Bahari ya Hindi ambacho kinahisiwa huenda kikawa na uhusiano na ndege ya Malaysia iliyopotea.
Picha za Satellite kutoka kituo cha utafiti cha Marekani kikionyesha eneo ambako msako…

Picha iliyotolewa na vyombo vya habari vya China vikionyesha kitu kipya kilichogunduliwa na satellite za nchi hiyo kikielea katika Bahari ya Hindi ambacho kinahisiwa huenda kikawa na uhusiano na ndege ya Malaysia iliyopotea.
Picha za Satellite kutoka kituo cha utafiti cha Marekani kikionyesha eneo ambako msako mkali unaendelea kuitafuta ndege iliyopotea huko katika bahari ya Hindi.
Hussein aliwaambia waandishi wa habari jijini Kuala Lumpur: 'Balozi wa China amepokea picha ya kitu kinachoelea kusini mwa bahari ya Hindi na amesema watatuma meli kuchunguza.
Muakilishi wa Waziri Mkuu wa Australia Warren akiongea na waandishi wa habari RAAF Pearce Base.
Ofisa wa anga, Peter Moore, ambaye pia ni rubani, amesema mchanganyiko wa hali ya hewa nchi kavu na ile ya bahari unaathiri ndege za uokoaji.
•    Waziri wa Mawasiliano Malaysia atangaza picha mpya ya Satellite
•    Asema China imetuma meli kuchunguza
•    Ni wiki mbili sasa tokea ndege hiyo ipotee
Kipande kikubwa cha chuma kimeonekana kikielea katika bahatri ya Hindi. Picha za Satellite za China zimeona  kipande chenye urefu wa futi 72 kiasi cha maili 75 mashariki mwa Australia.
Picha hizo zimechukuliwa siku mbili tu baada ya mamlaka za Australia kuona kitu kinachoelea katika pwani ya bahari ya Hindi

src
GPL

Wednesday, March 12, 2014

Wahadhiri wa vyuo vya umma wagoma Kenya

 



Wahadhiri wanadai kulipwa nyongeza ya mishahara
Mafunzo katika vyuo vikuu vya umma nchini Kenya yameathirika baada ya wahadhiri wa vyuo kuanza rasmi mgomo wa kitaifa.
Wahadhiri hao wamekiuka agizo la mahakama na kutogoma na kuamua kugoma.
 
Wanailaumu serikali kwa kutotekeleza makubaliano ya nyongeza ya marupurupu yao kama ilivyoahidi mwaka jana.
Mgomo huo unajiri wakati serikali ya Kenya imewataka wafanyikazi wa serikali kukubali mishahara yao kupunguzwa hasa baada ya Rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto pamoja na baraza la mawaziri kupunguza mishahara yao kutokana nagharama kubwa ya matumizi ya serikali.
Zaidi ya wafanyakazi 30,000 wa vyo vikuu wameanza kususia kazi baada ya waziri wa elimu kukosa kufikia makubaliano ya kusitisha mgomo huo ambapo wahadhri wanadai shilingi bilioni 3.9 kati ya wahadhiri na wakuu wa vyuo hivyo.
Kwa sasa idadi ya wanafunzi ambao watakosa mafunzo ni kati ya 200,000 na 300,000, ikiwa serikali haitaleta suluhu.
Mkutano wa awali kati ya waziri wa elimu na makatibu wake wawili, haukuzaa matunda.
Kiini cha mgogoro huo ni malipo ya awamu ya pili ya shilingi bilioni 7.8 ya nyongeza ya mishahara ambayo iliafikiwa mwaka 2012.
Pesa hizo zilipaswa kulipwa kwa awamu, huku nusu ya pesa hizo zikilipwa Disemba mwaka 2012.