
Macho
na masikio ya Watanzania wengi kwa siku ya Jumamosi June 07 yote
yalielekezwa Durban Afrika Kusini sehemu ambako zilikua zikitolewa tuzo
za wateule wa MTV Afrika Music Award ‘MAMA’.
Furaha
tuliyokuwa nayo Watanzania ilikua kubwa baada ya kuona kijana kutoka
nyumbani Tanzania kuwa ni miongoni mwa vijana wanaochuana kwenye tuzo
hizo tena akiwa vipengele viwili,ingawa bahati haikua njema kwa Diamond
kwani hakufanikiwa kupata.
Baada
ya kutangazwa washindi hao na yeye kutokuwepo Dimaond Platnumz
ameandika maneno haya kwenye kurasa zake za mitandao ya
kijamii>’Maisha ni Hatua.. Nafkiri kwa mwaka huu ile ndio ilikuwa hatua yetu kwa MTV…Cha muhimu ni kujua wapi tulipokua mwaka jana na wapi tulipo leo… pia kujifunza na kujua ni nini cha kuongeza zaidi ili Next tym tuzidi kufanya vyema…. Shukrani zangu nyingi ziende kwa Mashabiki wote,Management, Media,Family, wasanii na wadau Mbalimbali kwani kwa nguvu zao ndio zimefanya leo kunisogeza toka sehem moja kwenda nyingine…Next stop #BET!!!… Asante sana #Sheriangoi kwa Suti Hii’. Diamond Platnumz alikuwa pia ni moja kati ya watumbuizaji wa ugawaji wa tuzo hizi,ambapo kwa namna alivyoingia kwenye jukwaa na Davido ilimfurahisha kila mtu aliyekuepo ukumbini na watu waliokuwa wakiangalia nyumbani kupitia DSTV.





