MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, ametaja kilichoinyima ushindi mkubwa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars), ilipocheza na Zimbabwe wikiendi iliyopita.
Stars ilivaana na Zimbabwe kwenye mchezo wa awali wa kutafuta tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika na kupata ushindi wa bao 1-0.
Akizungumza na Championi Jumatano, Kabwe alisema Stars ilicheza mchezo mzuri na wa kuvutia lakini tatizo kubwa lilikuwa sehemu ya kiungo ambayo ilikuwa ikiongozwa na Frank Domayo ambaye mara nyingi alionekana kuchoka.
Straika tegemeo katika kikosi cha Taifa Stars, Mbwana Samatta.
Alisema pia safu ya ushambuliaji ilikosa mabao mawili ya wazi ambayo kama wangetumia nafasi hiyo vizuri, anaamini wangeibuka na ushindi mkubwa.“Tunashukuru tumeshinda hapa nyumbani, tunaenda ugenini, nafikiri wenzetu walituzidi sana kwenye safu ya kiungo, hivyo ni vyema mwalimu akaliangalia hili mapema kwani tunaenda kwao.
“Katika ushambuliaji niliona Mbwana Samatta alikosa kama mipira miwili hivi ya kumalizia, kama tungeitumia tungepata ushindi mkubwa, lakini hayo yamepita, nafikiri mwalimu atakuwa ameona upungufu kabla ya kwenda kurudiana,” alisema Zitto
src
GPL