KUNA mjadala mkubwa juu ya takwimu za Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kwa kweli, Bunge Maalumu la Katiba likikosa umakini kwenye eneo hilo, mchakato wa Katiba Mpya unaweza kukwama kabisa.
Kama tukiangalia kiyakinifu takwimu za tume, tutakubaliana kuwa zinapaswa kupuuzwa na nitaeleza bayana kama kama ifuatavyo.
Kukosa nguvu ya kisheria
Ukweli ni kuwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba haikuelekeza tume kuendesha kura za maoni. Kura za maoni zingefanyika zingekuwa zimebeba uamuzi wa umma na sio tena mapendekezo. Kungekuwa hakuna mjadala tena juu ya uamuzi wa umma. Tume kama iliona kuna umuhimu ingeweza kupendekeza mabadiliko ya sheria ili kuweza kupata takwimu halali zisizo na mawaa ambazo zingezitumika namna zinavyomitumika sasa.
Pamoja na hayo tume haikuwa na rasilimali, miundombinu wala weledi wa kufanya kazi ya kukusanya maoni kwa misingi ya kitaaluma. Cha ajabu tume inatumia takwimu zake kana kwamba ni uamuzi wa umma wakati kihalali ni mapendekezo ya kikundi kidogo cha watu. Kuna tofauti kati ya maoni na uamuzi.
Mchakato mbovu wa kupata takwimu
Hebu kwanza tunukuu sehemu ya hotuba ya Warioba bungeni kipemgele 101 cha hotuba kinasema: "Pia tume ilijadili njia bora ya kupata maoni. Tume ilifikiria kuandaa dodoso ili wananchi wajibu maswali mbalimbali kuhusu Katiba. Hata hivyo, tume iliamua wananchi wasipewe mwongozo ili wawe huru kusema chochote wanachoamini. Msingi huu ndio ulifuatwa na tume kupata maoni ya wananchi katika maeneo yote, ikiwa ni pamoja na suala la Muungano.”
Kwa nukuu hiyo, tayari tume ilikwishafanya uamuzi kutotumia takwimu kiyakinifu. Tayari walikuwa hawana mamlaka wala maelekezo ya kisheria bado walikuwa na nafasi kukusanya takwimu kwa namna bora zaidi. Uamuzi wa kutotumia dodoso maana yake walikuwa wameamua kukusanya maoni kwa njia ya “mnada”. Ni sandakalawe, wananchi pasipo maelekezo yoyote walizungumzia walichoona kipaumbele kwa muda mchache waliopewa pasipokujua wanashiriki katika kura za maoni!
Wananchi walikuwa huru kuzungumzia Muungano, maji, mirathi na masuala mengine ndani ya muda uliopangwa. Kwa msingi huu ni uongo kusema tume ina uamuzi au hata maoni ya umma ya kina juu ya Muungano au jambo jingine lolote. Ndio maana haishangazi kuwa pungufu ya asilimia 14 ndio waliozungumzia Muungano kati ya wananchi wote waliotoa maoni yao.
Watetezi wa mfumo wa Serikali tatu wanakosea kufananisha takwimu hizi na kura za urais. Kwamba Rais amechaguliwa na watu milioni tano lakini anaongoza watu milioni 45. Sio sahihi kufananisha mifano hii. Kwanza uchaguzi wa Rais huwa sio siri, taratibu zinaeleweka mpaka namna ya kutangaza matokeo.
Tume ilikusanya maoni kiholela baadaye wakatangaza "matokeo" ili kuipa nguvu hoja yao ya Serikali tatu, hapo mwanzo hapakuwa na maelekezo yoyote kuwa tume inaendesha kura za maoni juu ya muundo wa Muungano. Pili, njia sahihi kufananisha takwimu za tume na uchaguzi wa urais uko kwenye kura zilizoharibika, ni sawa na kusema kila watu kumi, kura tisa ziwe zimeharibika, hii ndio tafsiri sahihi ya ulinganifu wa takwimu za tume na matokeo ya urais. Au katika chumba cha kupigia kura, mwananchi aingie katika chumba cha kupigia kura kisha anapewa karatasi moja ya kupigia kura inayomtaka kupiga kura pasipo maelezo ya wadhifa wa kiongozi anayemtaka, wananchi tisa wanaamua kumchagua mbunge, mmoja anachagua Rais, halafu matokeo ya urais ndio yanatangazwa tena kwa hoja ya wengi wape! Tume ilikwishafanya uamuzi wa kutotumia takwimu ila baadaye kwa misingi ya kuuza uamuzi wa tume sasa wanalazimisha kusema wamebeba sauti ya wengi.
Serekali tatu ni utafiti wa tume?
Kwenye hotuba ya Warioba anakiri walifanya utafiti. Ni vigumu kuelewa kwa nini hawakuwapa wananchi utafiti wao kwanza kabla ya kuchukua maoni yao. Tume ilifanya utafiti baada ya kukusanya maoni na hatimaye kupendekeza muundo waliopendekeza. Na hata walipomaliza kufanya utafiti walifanya maridhiano, tena wanatuambia walifikia maridhiano pasipo kupiga kura. Ni vigumu mno kubainisha kwa kiwango gani pendekezo la tume ni matokeo ya maoni ya wananchi, ni kiwango gani cha matokeo ya utafiti na ni kiwango gani matokeo ya maridhiano ya wajumbe wa Tume. Kwa mchanganyiko huo ni vigumu kusema moja kwa moja kuwa pendekezo la Serikali tatu ni matokeo maoni ya umma. Pia tume ilikuwa huru kuchambua maoni ilivyoona inafaa, kufanya tafiti walizochagua wenyewe na hata kuandika kwa utashi wao. Ushiriki wa umma katika utafiti na uandishi haukuwepo, hivyo sehemu kubwa ya matokeo ya muundo uliopendekezwa ni mtazamo wa jumla wa tume na sio umma.
Takwimu kutumika eneo moja tu
Katika sehemu niliyonukuu hapo awali tumeona kuwa Tume ilitumia msingi mmoja wa kukusanya maoni katika maeneo yote. Cha ajabu, tume inaongelea takwimu za idadi ya Serikali tu, haionyeshi takwimu za umma juu ya mambo ya Muungano waliyopendekeza, hakuna takwimu za umma juu ya kuua Muungano na kuunda shirikisho na maeneo mengine yaliyowapendeza katika maeneo mengine. Hii inaleta mashaka juu ya ubora wa takwimu zilizotumika kwa minajili ya zilivyopatikana na uhalali wake.
Takwimu zinategemea mtumiaji
Kwa sababu msingi wa takwimu umekosa ubora wa kitaaluma, mtu yeyote anaweza tafsiri takwimu kukidhi malengo yake. Tumeona Warioba akikokotoa kwa kutoa idadi ya walioshiriki kutoa maoni ili kupata asilimia alizotaka na Profesa Issa Shivji akikokotoa kwa ujumla, maoni yote na hivyo kubainishi ni asilimia tano tu ya waliotoa maoni ndio walipendelea Serikali tatu, Rais Kikwete pia alitumia njia hii.
Hata kwa njia ya Warioba hupati jawabu alilopata yeye Warioba ili kufikia alipotaka, aliamua kutafsiri asilimia 60 za pendekezo la Muungano wa mkataba kama pendekezo la Serikali tatu. Wakati pendekezo lenyewe linazungumzia mfumo na sio muundo. Kutokana na udhaifu wa msingi uliotumika katika kupata takwimu na utata wake ni makosa kuzitumia takwimu katika kufanya uamuzi mkubwa.
Dhana inakataa ya takwimu
Tunaelewa kuwa Bunge Maalumu la Katiba ili kupitisha ibara yoyote na Katiba kwa ujumla, inahitaji kupitishwa na theluthi mbili za wabunge wa kila upande wa Muungano. Kihesabu, theluthi mbil ni asilimia 67. Msingi wa maoni ya tume juu ya Serikali tatu ni asilimia tano tu ya waliotoa maoni. Sasa msingi dhaifu wa asilimia tano haupaswi kubeba paa la asilimia 67. Ukuta na paa unakuwa mzito mno katika namna ambayo msingi hauwezi kuubeba.
Serikali tatu na ufafanuzi wa Warioba
Warioba alianza kueleza kuwa Muungano uliochwa na waaasi sio huu tulionao. Muungano wa Waasisi ulikuwa wa nchi moja sasa hivi kuna nchi mbili. Maelezo haya na kwa namna yalivyowasilishwa na Warioba hayaonyeshi kama msingi wake ni takwimu bali ni hisia na man’gamuzi yake binafsi au ya tume kwa ujumla wake. Pia aliorodhesha matukio ya kihistoria, ambayo baadhi yalipotoshwa kukazia lengo lake pamoja na kinachoitwa kero za Muungano na ripoti za Tume ya Nyalali na ile ya Kisanga. Kama msingi wa pendekelezo la Serikali tatu ni umma hakukuwa na haja kubwa ya kufanya utafiti katika kufikia hitimisho ambalo limekwishaamuliwa na umma. Mwenyekiti wa Tume pia hakuwa makini kabisa kuzungumza maneno kama “suluhisho pekee ni hili” na “muundo wa Serikali mbili hauwezekani”, haya yalikuwa ni matumizi mabaya ya fursa aliyokuwa nayo na alijenga msingi mbaya wa maridhiano bungeni. Itakumbukwa kuwa hapo kabla Warioba alifanya jaribio la kulipa Bunge Maalumu taswira ya chombo cha uhariri kisicho na mamlaka yoyote ya kubadili maandishi ya tume, kwa mtazamo wake, Bunge ni dhaifu kwa tume kimamlaka.
Kwa kudhamiria, alikataa kutambua kazi ya Tume ilikuwa ni kuandika rasimu wakati ya Bunge ndio hasa lenye jukumu la kutunga Katiba.
Mchakato haujabeba maridhiano
Tunaelewa kuwa tume iliendesha “mnada” wa maoni na hatimaye kutoa rasimu ya kwanza na baadaye Mabaraza ya Katiba. Hapakuwa na elimu pana kwa umma juu ya Katiba na masuala mazito kama ya Muungano wala mijadala na midahalo. Tume ilihodhi mchakato mzima wa Katiba na wakihofu sana ushiriki wa wanasiasa. Ni mjadala ambao ulikuwa umefungwa sasa umefunguliwa.
Kwa namna ambavyo mchakato uliendeshwa hapakuwa hata na makubaliano wala maridhiano kati ya wilaya na wilaya, hakuna makubaliano na maridhiano kati ya Kinondoni na Ilala, Kasulu na Kibondo, Pemba Kusini na Kaskazini au Unguja Kaskazini na Kusini, ni nyaraka inayojumuisha mapendekezo ya ngazi ya wilaya yaliyotokana na msingi mbovu wa rasimu ya kwanza. Kwenye Bunge Maalumu, Tanzania haiangaliwi kama jumuisho la wilaya bali kama taifa. Pande mbili za Muungano katika Bunge Maalumu zitajadiliana na hatimaye kufikia maafikiano, hivyo mitazamo yote inapaswa kupimwa na kujadiliwa.
Kama tulivyoeleza tunaweza kuhitimisha sasa takwimu za timu hazina uhalali kwa vigezo vyote, ubora, sheria na mantiki. Mwenyekiti wa Tume na sasa “UKAWA” wanatumia kama mkakati na sanaa ya kimasoko katika kuuza ajenda ya Serikali tatu kwa kisingizio kuwa ni chaguo la umma pasipokuwa kuwa na ushahidi wowote ule. Ni matumizi ya nguvu kushinikiza rasimu ya tume imebebea maoni sembuse uamuzi wa umma. Kwa namna wanavyoshinikiza na kielelezo cha uoga kuingia kwenye mjadala wa wazi na kukabili changamoto halisi za Muungano. UKAWA waache uoga, wasijifiche kwenye “uamuzi” wa umma ambao hawana. Walete hoja, tuzisikie. Naamini kwenye rasimu, UKAWA wana maeneo mengi tu watakuwa wana mapendekezo ya kuyabadilisha ila kwenye muundo wamechagua kujificha kwenye msingi mwepesi wa tume, hizi ni hila na haziwezi kutupatia Muungano imara. Tunashukuru Rais Kikwete ameweza kufungua mjadala ambao Warioba alitaka kuufunga. Sasa tujadili muundo na mfumo wa Muungano hoja kwa hoja, umma bado haujafanya uamuzi na tukatae matumizi
src
Raia mwema