Saturday, March 1, 2014

ZEE LA NYETI: Kila kwenye kula, kuliwa kunahusika

Kuna mchongo nimeletewa na wana, uko mtandaoni, unaambiwa kuna websaiti ukijiunga hiyo, kila anayejiunga baada yako, ni mkwanja,  nataka niingie kwenye huu mchongo ila nina wasiwasi kidogo, sijui mbele kuna mizingulizi kudadadeki?

Manake si unajua tena tauni? Hizi ishu zinazotengeneza mkwanja kirahisi bila kuzikodolea macho, unaweza kujikuta unakung’utishwa mpaka nauli ya kuibukia jobu.

Bongo unaionaje bwanangu?

Nuksi

Ishu kama hizi, mwisho wa siku unaweza kujikuta akiambiwa utoe akaunti namba na paswedi, baada ya siku mbili tatu, watu wanalamba mpaka kiakiba chako, unabaki unachachawa tauni, watu wanakucheka tu, tena kwa Zarau kudadadeki.

Moyo wangu umesita mwanangu mwenyewe, nimeamua kuingia kitaani kuzisaka kwa kutumia akili na nguvu siyo kirahisi hivi au siyo mwanangu?
Lakini hata ukizipata hizo pesa, pia unatakiwa kuwa makini, maana Bongo ukizubaa tu unaachwa feri.

Unafikiri juzi mwanetu Buchwaka kafanywaje?

Unaambiwa, mchizi kaingizwa kingi hivi hivi na watoto wa kiMeru kutokana na ushamba wake wa mademu. Jamaa sijui kashuka lini kutoka Bwiti, basi kajaa mzima mzima, kuja kushtuka, watu zamaaaani washajilia vyao.

Unajua kilichomponza nini?

Hizi zetu za kila ukiona mtoto mzuri unajifanya kutaka kumuamini kupitiliza, ndiyo unajikuta kama unazinguka hivi.

 Unajua nilichokishtukia kwa laifu ya sasa, hawa watoto wetu ni bora tuwape muda wa kuwaona hawa watoto wazuri mapema, ili ukubwani wasije wakazinguka kama mchizi
Mwanetu yaani alidata kwa sekunde chache na katika sekunde chache hizo hizo akapigwa, kitu kama M hivi na watoto wa Kimeru halafu watu haooooo.

Kwani nini bwana?

Si ushamba wake mwenyewe?

Unajua ilikuwaje?

Jamaa katua Arachuga bwana kwenye kihoteli flani cha kitaa na mkwanja wake wa biznes, katika hangaika hangaika yake, pale pale ndani si unajua mambo ya rum sevis na nini, akakikwaa kitu cha Kimeru, unaambiwa kiko fulu kwa kukiangalia, tatizo kichwani sasa ndiyo mchizi hakujua kilikuwa kinawaza nini. Si unazishtukia zile za kuangalia kasha la simu halafu ukaiona ni kiboko, kumbe mchina kashamaliza shughuli?

Ndiyo kilichomkuta, alivyoona sare za hoteli zimemkaa kimwana, mchizi akajua haswaaaaa, hapa ndiyo nilipokuwa nikipatafuta mie walaah, akataka kujiweka. Kwani binti alikuwa na noma basi, akawa anamsikiliza tu jamaa kajielezaaaaaa, mpaka mabiashara yake mpaka kaja na kiasi gani na nini, binti akaona fresh, akamwambia mwana usikonde, mida mida ntakushtua nipe namba,mwana akatoa!
Kudadadekli

Midamida inaelekea kama binti aliwashtua wana hivi, akawaambia kwamba kuna mliga kama kaingia kingi hivi, inabidi watu kama washughulikie mradi ili mwisho wa siku wakae mezani wagawane kilichopo.

Dizaini kama ilikuwa ngumu hivi binti kuipiga ishu peke yake akaona bora kama aigawanye, ili yaliyomo yawamo kama yatakuwa yanataka kumwagika ikiwezekana yamwagwe....

Uliza muvi lenyewe sasa lilivyopigwa!

Demu kamwambia mchizi kwamba siwezi kuspendi na wewe kwenye hii sehemu yangu ya kuwajibika twenzetu hivi walipoibuka samwea baada ya gambe sana, wakaibuka wana, wakadai kwamba mchizi kawachukulia demu wao, wakaanza kama kutaka kumpa mwana kichapo hivi. Mara akaibuka mwana mwingine kama anamtetea hivi, haukamu mchizi abondwe, watu wakadai kama wanataka asidhurike nini awatoe na mkwanja, ndiyo mwana akaulizwa una ngapi hapo?

Kudadadeki, kabla hajajibu watu wakamkung’utisha everisingi,
wakasepa.

Na hadithi yangu ikaishia hapo, Jumamosi njema, utaniambia umejifunza nini kwenye FaceBook FanPage ya Zee la Nyeti...

src
mwananchi