- Vyovyote vile, kuwabembeleza Wazanzibari kuna ukomo
MENGI yamesemwa na kuandikwa kuhusu hotuba ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa Ijumaa iliyopita, mjini Dodoma, wakati akifungua rasmi kikao cha Bunge la Katiba.
Nami niungane na wale wote waliosema kuwa kuna mambo ambayo Rais Kikwete hakupaswa kuyasema au kuyawekea msimamo wakati wa hotuba yake ya ufunguzi.
Katika suala la muundo wa Muungano, kwa mfano, Rais Kikwete alipaswa tu kuishia katika kuwaeleza wajumbe wa bunge hilo maalumu uzuri na ubaya wa kubakia na mfumo wa serikali mbili na uzuri na ubaya wa mfumo unaopendekezwa wa serikali tatu, na kuachia wajumbe wa Bunge hilo kuamua wenyewe ni upi wanaoutaka.
Lakini yeye sivyo alivyofanya; kwani alienda mbali na kueleza ‘hisia’ zake binafsi kuwa mfumo unaofaa ni wa serikali mbili, na hata kufikia hatua ya kuuponda mfumo wa serikali tatu na kusema kwamba wanaoutaka wasubiri kwanza aondoke madarakani!
Sote tunajua kwamba kama Rais wa nchi, ‘hisia’ zake hizo binafsi ni maelekezo yasiyo rasmi kwa wajumbe wa Bunge hilo wapinge kwa nguvu zote pendekezo la mfumo wa serikali tatu lililopo kwenye rasimu ya Katiba.
Tukizingatia kwamba idadi kubwa ya wajumbe wa Bunge hilo la Katiba ni kutoka CCM, na Rais Kikwete ndiye Mwenyekiti wa chama hicho, ni dhahiri kauli yake ni maelekezo rasmi, na kwamba uamuzi ni serikali mbili hata kabla Bunge hilo maalumu halijapiga rasmi kura kuamua.
Isitoshe, kauli yake kwamba wanaotaka serikali tatu wasubiri kwanza aondoke madarakani; maana yake ni kwamba hayupo tayari kuukubali mfumo huo hata kama wajumbe wa Bunge hilo wataupitisha. Kama hivyo ndivyo, aliunda Tume ya Katiba ya nini? Na Bunge la Katiba la nini kama haliko huru kuamua linayotaka?
Hata kauli yake ile nyingine kwenye hotuba yake kwamba Serikali ya Muungano (kama Serikali ya Tanganyika itaundwa) itakuwa haina mapato, na hivyo wanajeshi wanaweza kukosa mishahara, na hivyo kuzipindua serikali shiriki (ya Tanganyika na Zanzibar), ililenga katika ‘kuwatisha’ wajumbe na kuwaingiza hofu ili wapige kura kukataa pendekezo la serikali tatu. Je, hiyo ilikuwa sahihi kwa Rais wa nchi kuwatisha wajumbe wa Bunge la Katiba?
Mzee Pandu Kificho naye alikuja kuharibu kabisa mambo wakati wa hotuba yake ya kumshukuru Rais Kikwete kwa kulifungua rasmi bunge hilo pale alipoisifu hotuba hiyo kwamba ilikuwa ni ya kushauri, kufafanua na ‘kuelekeza’. Neno ‘kuelekeza’ hakupaswa kabisa kulitamka; maana hakuna popote pale duniani ambako Rais wa nchi ‘anaelekeza’ wajumbe wa Bunge la Katiba nini cha kukubali na nini cha kukataa katika kuandika Katiba mpya!
Nasisitiza kwamba wako walioshangazwa na maudhui ya hotuba ya Kikwete katika kipengele cha rasimu ya Katiba kinachohusu suala la Muungano, lakini mimi si mmoja wao. Alishaonyesha dalili hiyo.
Tunaofuatilia, kwa miaka kadhaa sasa, hulka na utendaji kazi wa Rais Kikwete, tulishaona mapema dalili kwamba katika hotuba yake hiyo angeelekeza “kisanii” Bunge hilo la Katiba kukataa pendekezo la Tume ya Warioba la serikali tatu.
Hata kule kumtanguliza Jaji Warioba kuwasilisha kwanza rasimu ya Katiba, na ndipo yeye (Kikwete) aende kulifungua rasmi bunge hilo ulikuwa ni “usanii” wa aina yake wa kumpa fursa ya kuliponda pendekezo hilo la serikali tatu la Tume ya Warioba mbele ya Bunge hilo la Katiba.
Ili kuwaridhisha wana CCM wenzake, Kikwete si tu aliikosoa Tume ya Warioba kwa kuibuka na rasimu inayopendekeza muundo wa serikali tatu, lakini alifikia hata hatua ya kuzitilia shaka takwimu za tume hiyo zilizopelekea kupendekeza aina hiyo ya muundo wa Muungano.
Swali la kujiuliza: Kwa nini maoni yake hayo ‘binafsi’ hakuyatoa kwa Tume wakati ilipokuwa ikipokea maoni ya wananchi mbalimbali, na badala yake alisubiri kuyatoa katika kikao cha Bunge hilo la Katiba kwa namna ya ‘kuelekeza’ nini kikubaliwe na nini kikataliwe? Je, huko si kuidhalilisha mbele ya umma kazi nzuri iliyofanywa na Tume hiyo?
Mtazamo wangu mimi ni kwamba Kikwete tangu mwanzo hakuwa na dhamira thabiti ya kuipa nchi Katiba mpya inayotakiwa na wananchi. Alitaka tu kuingia katika vitabu vya historia kama Rais alijeipa nchi Katiba mpya; hata kama Katiba hiyo siyo iliyotakiwa na wananchi!
Vinginevyo, asingelishinikiza Bunge la Katiba likatae pendekezo la kuwa na mfumo wa Muungano wa serikali tatu kwa kauli yake ile kwamba wanaoitaka wasubiri kwanza aondoke madarakani!
Kwa ufupi, huyo ndiye Rais Kikwete. Huwa wakati mwingine hatabiriki, haeleweki na anakanganya, na vyote hivyo huigharimu nchi.
Kwa kuwaeleza wajumbe ‘hisia’ zake hizo binafsi za kuunga mkono muundo wa serikali mbili, na si tatu zilizopendekezwa na Tume ya Warioba, sasa kile kiporo cha kanuni cha iwapo upigaji kura kupitisha vifungu vya rasimu hiyo uwe wa siri au wazi, kitakuwa kigumu zaidi kuamua baada ya hotuba hiyo ya Kikwete, na sitashangaa Bunge hilo likivunjika kwa kushindwa kufikia mwafaka juu ya kipengele hicho cha kanuni.
Hilo likitokea, mapesa ya walipakodi yatakuwa yametafunwa bure tu na wajumbe wa Bunge hilo la Katiba, na huo ndiyo msingi wa kauli yangu kwamba mikanganyiko ya Kikwete wakati mwingine huligharimu Taifa!
Nihitimishe tafakuri yangu kwa kuwaleteeni mawazo ya Mtanzania mmoja (au Mtanganyika mmoja!) anayejiita Ng’wamapalala aliyoyaweka katika mtandao wa jamiiforums, Machi 22, kuhusu hotuba za Jaji Warioba na Rais Kikwete ndani ya Bunge hilo la Katiba.
Mwananchi huyo amekerwa (na nakubaliana naye) na namna ambavyo hotuba za wawili hao – Warioba na Kikwete za namna ya kumaliza matatizo ya Muungano zilivyoonekana ‘kuwabeba’ Wazanzibari bila kuzingatia sana hisia za Wabara. Mwananchi huyo aliandika hivi:
“Nilijaribu kuwasikiliza viongozi wetu kuhusu suala la Muungano, lakini nimeguswa na mantiki za hoja zao katika kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya Muungano.
Tume ya Jaji Warioba ilifikia makubaliano kuwa kuyatafutia ufumbuzi malalamiko ya Wazanzibari ni kuponya matatizo ya Muungano bila kujali matatizo ya watu wa Bara. Hata hoja ya serikali tatu ilikuwa imebebwa na utatuzi wa malalamiko ya Wazanzibari, na si Wabara.
Jaji Warioba kwenye hotuba yake ya Bunge la Katiba katika ukurasa wa 39, namba 122, alisema, (ninanukuu);
‘Tume iliamua kufanya uchambuzi wa kina kuhusu baadhi ya malalamiko, hasa malalamiko ya Zanzibar. Malalamiko ya Tanzania Bara yanatokana, kwa kiwango kikubwa, na hatua zilizochukuliwa kwa upande wa Zanzibar. Kama malalamiko ya Zanzibar yakipatiwa ufumbuzi, malalamiko ya Tanzania Bara nayo yatakuwa yamepatiwa ufumbuzi.’
Hata hotuba ya Rais Kikwete nayo pia ilijikita katika kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya Wazanzibari kama ndiyo ‘mwarobaini’ wa matatizo pekee ya Muungano.
Rais Kikwete ameainisha matatizo ya Wazanzibari katika kujenga hoja ya serikali mbili; kana kwamba kuyatafutia ufumbuzi malalamiko ya Wazanzibari ndiyo ‘mwarobaini’ wa matatizo ya Muungano!
Je, hii imekuja kwa sababu ya kelele nyingi za Wazanzibari au kwa sababu, kama watu wanavyodai kuwa, tumewashinikiza au tumewalazimisha Wazanzibari kuwepo kwenye huu Muungano, na kinachofanyika kwa sasa ni ‘kuwabembeleza’ kwa kuwapa kile wanachokitaka ili wabakie kwenye Muungano?
Je, hii ni kwa sababu ya ukimya wa Watanganyika katika kuyapigia kelele matatizo ya Muungano kwa upande wao ndiyo maana Tume ya Jaji Warioba haikuona umuhimu wa malalamiko yao kupewa fursa sawa na malalamiko ya Wazanzibari?
Na hata hotuba ya Rais Kikwete imefanya kile kile ambacho Tume ya Jaji Warioba imekifanya kwa kuyaweka chini ya kapeti malalamiko ya watu wa Bara katika kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya Muungano kwa sababu ukiangalia hotuba ya Rais Kikwete ilikuwa inajibu hoja za Jaji Warioba kwenye Rasimu ya Pili ya Katiba.
Je, unadhani hii dhana ya 60% kwa watu wa Zanzibar kutaka Muungano wa mkataba (kwa maana nyingine wanataka kuvunja Muungano) ndiyo imewafanya viongozi wetu wayachukue malalamiko ya Wazanzibari kwa uzito zaidi kuliko 61% ya watu wa Bara waliotaka kimantiki Muungano uendelee kuwepo katika serikali tatu?
Nini kiko nyuma ya hii mantiki ya viongozi wetu kuangalia kwa uzito malalamiko ya Wazanzibari badala ya malalamiko ya pande zote za Muungano kuyaweka katika mzani wa usawa?”
Hivyo ndivyo alivyoandika Ng’wamapalala katika post yake kwenye jamiiforums. Anahoji mambo kwenye hotuba za Warioba na Kikwete kuhusu suala la Muungano ambayo yanafikirisha; nami nakusihi uyatafakari.
Kama kero za Muungano zinatatuliwa kwa kigezo cha kuwaridhisha Wazanzibari tu na si Wabara, swali la kujiuliza ni hili: Wabara ‘tutawabeba’ na ‘kuwabembeleza’ Wanzanzibari wabaki katika Muungano hadi lini?
src
Raia Mwema