JEAN Mwenda Bosco hakukosea hata kidogo alipoimba: “Kumbe kweli safari taabu.” Safari tuliyo nayo ya kupata Katiba mpya itayoyaridhia matakwa ya Watanzania wengi ni ndefu na ni ya taabu, tena ni ya taabu kwelikweli.
Safari hiyo inafanywa iwe ya taabu na ndefu kwa makusudi. Wenye kufanya hivyo ni watu fulani nchini Tanzania wanaoamini kwamba wao, na wao tu, ndio wenye haki ya kutoa maamuzi makuu kuhusu mustakbali wa Taifa. Jamaa hawa wanajihisi kwamba wao ni wakereketwa halali wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na wanakitumia chama hicho kuyalinda maslahi yao.
Wapo, bila ya shaka, wakereketwa wengine wa chama hicho hicho wenye kuona mbali na wanaotambua umuhimu wa kuweka mbele Taifa badali ya chama chao. Mwenyekiti wa sasa wa CCM, lakini, si miongoni mwao.
Ilisikitisha kumsikiliza Mwenyekiti huyo, Rais Jakaya Kikwete, Ijumaa iliyopita, akiishusha hadhi yake alipokuwa akilihutubia Bunge Maalumu la Katiba wakati wa uzinduzi wake. Baadhi yetu tukidhani kwamba atatushangaza kwa kulihutubia Bunge hilo akiwa kama kiongozi wa Taifa na si kiongozi wa chama. Badala yake alizungumza kama Mwenyekiti wa CCM aliyekuwa kwenye jukwaa la CCM.
Hotuba aliyoitoa katika Bunge hilo ilizidi kututhibitishia kuwa Kikwete ni mwanasiasa wa kawaida tu. Hana sifa za kumfanya aonekane kwamba amewapiku wanasiasa wenzake.Kwa bahati mbaya, lugha yetu ya Kiswahili haina neno moja tunaloweza kulitumia kuwa tafsiri ya neno la Kiingereza ‘statesman’. Lakini tungekuwa nalo neno hilo tusingeliweza asilan kulitumia kumuelezea Kikwete.
Ingawa statesman ni mwanasiasa lakini kuna tafauti kubwa baina ya mwanasiasa wa kawaida na statesman. James Freeman Clarke, mwandishi wa Mmarekani wa karne ya 19, aliwahi kusema kwamba: “Mwanasiasa hufikiria uchaguzi ujao. statesman hufikiria kizazi kijacho.” Alichofanya Kikwete Ijumaa iliyopita ni kuvipuuza vizazi vijavyo kwa kuyaweka mbele matakwa ya chama chake yenye kuzingatia maslahi ya chama badala ya Taifa.
Mwanasiasa wa kawaida hujaribu kufanya mambo yatayomnufaisha binafsi, aghalabu kwa kupika majungu au kwa kufanya ghilba. Pia mwanasiasa wa kawaida huwa mbioni kuyapigania maslahi ya chama chake badala ya maslahi ya taifa kwa jumla.
Kwa upande mwingine statesman hata akiwa kiongozi wa chama cha siasa, huyaweka kando maslahi ya chama chake na badala yake hupigania maslahi ya nchi. Yule mwenye kuyaweka mbele maslahi ya nchi yake pasina kuyazingatia maslahi yake binafsi au ya chama chake ndiye awezaye kulinufaisha taifa.
Tafauti nyingine baina ya mwanasiasa wa kawaida na yule aliye statesman tunaweza kuiona katika dhamiri inayomfanya mtu azivae siasa. Mwanasiasa wa kawaida hutaka achaguliwe ili apate madaraka aweze kujistawisha binafsi na pengine yeye na chama chake.
Statesman huwa na ruwaza kuhusu taifa lake. Huwa anajua kwa nini anataka uongozi na akiupata uongozi huwa amekwishapanga atautumia vipi kulifanya taifa lake liwe bora zaidi. Huwa hayumbiyumbi wala habadili imani zake ingawa anaweza akabadili sera zake au za chama chake endapo kwa kufanya hivyo taifa litaweza kuwa imara zaidi, la haki zaidi au la ustawi zaidi.
Kiongozi aina hiyo huwa jasiri na huwa tayari kuchukua hatua zitazowanufaisha wengi katika nchi yake hata kama hatua hizo zitakwenda kinyume na sera za chama chake. Au hata kama zitamfanya achukiwe na baadhi ya vigogo wa chama chake.
Hivyo, kiongozi aina hiyo huwa anaona mbali. Hutambua kwamba ataweza kukabiliwa na matatizo ambayo lazima ayapatie ufumbuzi ili aweze kutimiza malengo yake. Huwa anayaamini hasa anayoyahubiri na ni mwiko kwake kutokutimiza ahadi zake.
Wanasiasa wengi huwa ni watu wasio na uadilifu, ama huwa na mazoea ya kusema uongo ili wapate ulwa au hutoa ahadi chungu nzima wapate kuchaguliwa lakini wanapochaguliwa tu huzisahau ahadi walizotoa. Hawazitimizi.
Kwa upande mwingine, wale walio na sifa ya ‘ustatesman’ daima huwa wanaliangalia taifa linakwenda wapi na nini wafanye kuhakikisha kwamba halendi kombo. Viongozi aina hiyo huwa na uweledi wa kisiasa na huonyesha busara katika uongozi.
Uzinduzi wa Bunge Maalumu la Katiba ulimpa Kikwete fursa adimu na adhimu ya kuonyesha uweledi wake wa kisiasa na busara yake katika kuliongoza Taifa. Kwa ufupi, ulimpa fursa ya kuuonyesha ulimwengu kwamba yeye nistatesman. Kwa bahati mbaya, Kikwete aliifujilia mbali fursa hiyo.
Alisaidiwa na ile ghilba na hila iliyotumiwa na Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba Samuel Sitta ya kumshurutisha Mwenyekiti wa Tume ya Katiba Jaji Joseph Warioba amtangulie Kikwete kulihutubia Bunge la Katiba ili baadaye Kikwete apate nafasi ya ‘kumkaanga’. Na hivyo ndivyo Rais alivyofanya.
Kikwete hakuonyesha uungwana kwa uamuzi wake wa kumsulubu Warioba, mtu aliyemteua mwenyewe akiamini kuwa ana uadilifu wa kutenda haki. Kikwete alimkebehi, alimkanyaga na kumpondaponda Warioba akilitoa maanani pendekezo la Tume ya Katiba la kutaka muundo wa Muungano uwe wa serikali tatu. Halafu akautetea muundo wa Muungano wa Serikali mbili unaoshikiliwa na chama chake.
Nionavyo ni kwamba uongozi wake Kikwete ni uongozi unaoweza kulihatarisha taifa. Amekuwa mithili ya dereva anayetoa ishara kama anapinda kushoto kumbe analielekeza gari kulia kwenye barabara kuu yenye magari yaendayo kwa kasi kubwa. Lazima atasababisha ajali.
Tumuelewe vipi Rais huyu? Kama miezi mitano hivi iliyopita waziri mmoja (jina ninalihifadhi) aliye chanda na pete na Kikwete alimdokozea msiri wake kwamba Rais anapendelea muundo wa Muungano wenye serikali tatu. Waziri huyo ambaye ni muumini wa Muungano wa serikali tatu, aliyasema hayo kwa msisimko akidai kwamba ni Rais mwenyewe aliyemueleza msimamo wake. Au tuseme labda huyo Waziri alimsingizia tu Rais wake? Sidhani.
Sasa ninayakubali yanayosemwa na walio karibu naye kwamba Rais huyu, kwa hakika, hana msimamo kuhusu masuala mengi yanayolihusu Taifa na kwamba anachokisema asubuhi hutegemea alimsikiliza nani usiku uliopita.
Viongozi wa sampuli hiyo vilevile huwa ni hatari. Na huzidi kuwa wa hatari unapowasikia wanamtaja Mungu au watu wa Mungu katika maamuzi yao.
Kwenye hotuba yake ya Ijumaa iliyopita, Kikwete alidokeza kwamba ameshauriwa na “mtu wa Mungu” — ambaye hakumtaja kwa jina — aukatae muundo wa Muungano wa serikali tatu. Matamshi haya yana mushkeli wake.
Kwanza siku zote tangu enzi za Mwalimu Julius Nyerere tumekuwa tukiambiwa kwamba Serikali ya Tanzania haina dini. Sasa ilikwendakwendaje ikawa Rais anakata maamuzi yake kwa kuzingatia nasaha anazopewa na mtu wa dini?
Isitoshe. “Mtu wa Mungu” ameutilia shaka muundo wa serikali tatu na inavyoonyesha Kikwete ameufuata ushauri wake na amelitaka Bunge la Katiba nalo liupe nafasi ushauri huo na liuzingatie. Kule Zanzibar watu wa Mungu walisema hawautaki Muungano lakini hawakusikilizwa. Badala yake walitiwa korokoroni na kufunguliwa kesi mbele ya Mahakama.
Hata hivyo, “Mtu wa Mungu” aliyezungumza naye Kikwete ametahadharisha kuhusu muundo wa Muungano wa serikali tatu lakini juzi tu mtu mwengine wa Mungu Askofu Martin Shao alinukuliwa akisema kwamba kwa miaka 50 iliyopita Serikali ingeweza kuondoa kasoro za muundo wa serikali mbili, lakini kwa sasa imechelewa.
Kuna watu wa dini wengi wenye mawazo kama hayo ya Askofu Shao. Kwanini ushauri wa “Mtu wa Mungu” wake yeye Kikwete tu ndo upewe uzito na wa watu wa Mungu wengine upuuzwe?

src
Raia mwema