Mfumo wa awali kuhusu Makamu wa Rais urejeshwe
KWANZA nampongeza Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Warioba na Tume yake kwa kazi nzuri waliyofanya katika mazingira magumu. Inasikitisha kusikia baadhi ya wanasiasa wakimjadili mtu badala ya kujadili hoja yenyewe. Niseme hao wamefilisika kimawazo?
Ugomvi ni juu ya pendekezo la serikali tatu. Wakati Muungano ulipokuwa unapingwa na kunyofolewa mbona hawakujitokeza kujibu hoja za wapinzani wa Muungano? Walikuwa wapi? Ukimya wao sio ishara ya kuwaunga mkono wapinzani hao? Je, walitaka Jaji Warioba atumie mabavu kama dikteta kwenda kinyume cha maoni ya wananchi na wenzake katika Tume? Hiyo ndiyo demokrasia?
Pili, baada ya hayo, niseme pia kwamba binadamu hawezi kuwa mkamilifu katika kutenda au kuamua mambo. Upo uwezekano pakawepo na upungufu na hivyo kukawepo nafasi ya kufanya masahihisho na kuboresha. Katika rasimu hii ya pili naona ina sehemu tatu. Sehemu ya kwanza ni maoni ya wananchi ambayo yameandikwa katika mfumo wa kisheria. Sehemu ya pili, ni maoni ya Tume yenyewe. Sehemu ya tatu ni baadhi ya mambo yaliyo katika Katiba ya sasa. Sitaingia katika uchambuzi wa maeneo hayo. Hata hivyo niseme ni muhimu kuheshimu maoni ya wananchi hata kama mtu hayataki na kama kuna uwezekano wa kuyaimarisha basi yaimarishwe. Lakini pia kwa nia ya kuboresha yale ya msingi isiwe haramu kuwa na mawazo tofauti na yale ya Tume yenyewe. Kwa mfano kuhusu orodha ya mambo ya Muungano, nafasi ya Makamu wa Rais, utaratibu wa kujaza nafasi ya Rais kabla ya kumaliza kipindi chake au wakati hayupo, utaratibu wa kupata wagombea urais au ubunge ili kupata wagombea wenye sifa, kumshtaki Rais, utaratibu wa kubadilisha Katiba na mengineyo. Naomba nitoe maoni yangu kwenye maeneo hayo ambayo lengo lake ni kuboresha na sio kuathiri msingi.
Mambo ya Muungano (ibara ya 63)
Ili kupata Serikali ya Muungano yenye nguvu na mamlaka ya kutosha, ipo haja ya kuongeza orodha ya mambo ya Muungano:
Yanayoweza kuongezwa ni masuala ya anga; mawasiliano; usafiri wa baharini. Maeneo hayo yanahusika na ulinzi na usalama wa taifa, hivyo napendekeza mambo hayo yawekwe chini ya mamlaka ya Serikali ya Muungano. Maeneo mengine ambayo ni muhimu yakadhibitiwa na Serikali ya Muungano ni misaada, mikopo (ibara 229) na madeni ya nje, lengo ni kuiwezesha Serikali ya Muungano kutimiza ipasavyo wajibu wake mkuu wa kulinda Jamhuri ya Muungano isichezewe na maadui wa nje au wa ndani.
Nchi inaweza kuuzwa kutokana na misaada mikubwa au mikopo iliyokidhiri kiasi cha kushindwa kulipa. Kuna nchi zilizopoteza uhuru wao kwa sababu hizo. Au nchi kuyumbishwa kwa sababu hiyo. Na nchi yetu imeonja hayo tulipotofautiana na “Wakubwa”. Pia tunaona jinsi baadhi ya nchi zilizoendelea zinavyoyumba kiuchumi kwa sababu ya kusongwa na madeni makubwa ya nje na sera bovu za uchumi , kwa mfano Ugiriki. Hivyo kama mshirika mmoja wa Muungano atafanya madudu huko madhara yake yataathiri taifa zima.
Bila shaka katika kutumia mamlaka hayo, Serikali ya Muungano sharti ishirikishe serikali za nchi washirika.
Wajibu wa kulinda Muungano
Tulipoingia kwenye mfumo wa vyama vingi vya siasa suala la jinsi ya kumpata Makamu wa Rais wa Jamhuri lilipasua vichwa vya watu. Mwishowe ikakubalika dhana ya mgombea mwenza wa mgombea kiti cha urais ambaye atakuwa Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Uamuzi huu pamoja na sababu zake zilizotolewa, uliacha pengo.
Rais wa Serikali ya Zanzibar hakuwa kiungo tena cha Muungano wa nchi mbili zilizoungana wala hakuwa tena na dhamana ya kuulinda Muungano kwa kiwango kilichostahili. Yaliyofuata baadaye huko Zanzibar ni hayo tunayoyashuhudia sasa hata kufikia hatua ya kupitisha Katiba yao ambayo imeingilia mamlaka ya Serikali ya Muungano kwenye maeneo mbalimbali ya utendaji na sera. Pia upinzani dhidi ya Muungano ukaongezeka kwa kasi ukisimamiwa na Viongozi wa juu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Maridhiano yaliyotokea kati ya Chama cha Wananchi (CUF) na Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar na yaliyofuatana nayo, yaliwezekana kwa sababu kiungo muhimu cha Muungano kutoka Zanzibar kilikosekana na kimekosekana. Iliwezekana kumvua madaraka Makamu wa Kwanza wa Rais, Aboud Jumbe kwa sababu kwa nafasi yake, alikuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano na Makamu wa Mwenyekiti wa CCM akiwa na wajibu mkuu wa wajibu wake wa kuilinda Katiba ya Muungano. Lakini alikuwa anafanya mambo ya kichini chini ya kudhoofisha Muungano mpaka alipofichuliwa.
Zile sababu zilizotumiwa kubadilisha kipengee hiki zilijengwa juu ya hofu ya kuwa “itakuwaje kama katika uchaguzi Rais na Makamu wake watatoka katika vyama tofauti- watafanyaje kazi kwa pamoja – huyu ni CUF na huyu ni CCM?” Kumbe duniani humu kuna serikali za mseto na serikali ya umoja wa taifa. Ili kuimarisha uwajibikaji na kuimarisha Jamhuri ya Muungano napendekeza mfumo uliokuwapo kuhusu nafasi ya Makamu wa Rais kabla ya kuingia kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa urejeshwe.
Utaratibu wa kujaza nafasi ya Rais kabla
Pendekezo kwamba; “Makamu wa Rais ataapishwa kushika madaraka ya Rais kwa muda uliobakia katika kipindi cha miaka mitano …”, kwa maoni yangu, halifai kwani linatoa nafasi kwa Ibilisi au adui wa nje au wa ndani kufanya njama za kumwondoa Rais aliye madarakani ili Makamu wake achukue nafasi hiyo. Kama inatokea na imekwishatoa mtoto wa mfalme kumpindua baba yake ili achukue ufalme wake, inawezekana kutokea pia kwa hili na kwa urahisi zaidi. Napendekeza kwamba nafasi ya Rais ikitokea kuwa wazi achaguliwe mwingine katika muda usiozidi miezi mitatu kama ilivyo katika Katiba ya sasa.
Utekelezaji majukumu ya Rais asipokuwapo
Mapendekezo kwamba; “Ikitokea nafasi ya madaraka ya Rais iko wazi kutokana na kazi… na shughuli za Rais zitatekelezwa na mmoja wapo wa wafuatao, kwa kufuata orodha kama ilivyopangwa.
Napendekeza kwamba nafasi ya Rais wakati hayupo isishikwe na mtu ambaye hakuchaguliwa na wananchi. Kufanya hivyo ni kudhalilisha nafasi hiyo. Hivyo kwa kuwa mawaziri hawatateuliwa kutoka miongoni wa wabunge, waziri yeyote hana sifa ya kushika nafasi hiyo.
KUHUSU SIFA ZA KUCHAGULIWA KUWA MGOMBEA NAFASI YA URAIS AU UBUNGE (IBARA YA 79 NA 125):
Kwa sasa vyama ndivyo vinavyopendekeza- kwa kweli kuteua mgombea. Kumbe baadhi ya walioteuliwa kugombea wasingechaguliwa kama wapiga kura wangewajua. Propoganda za vyama na mashabiki ndizo zinazotawala. Matokeo yake Taifa linapata viongozi wabovu na serikali dhaifu. Napendekeza kwamba pawepo na chombo cha kuchuja na kuhahiki sifa za wagombea waliopendekezwa na vyama. Kiwe na mamlaka ya kuyakataa na kuagiza vyama vipendekeze wengine au mwingine. Tume ya uchaguzi ipewe mamlaka hayo. Katika kutekeleza wajibu huu Tume itaongozwa na miiko ya uongozi iliyoorodheshwa katika Katiba hii. Zipo nchi nyingine zenye utaratibu huo wa kuchuja. Bila kuwa na chombo kama hicho sifa hizo zitabaki kwenye makaratasi na mambo yataendelea kama kawaida tulioizoea na Taifa litaendelea kupata viongozi wabovu.
BUNGE KUMSHITAKI RAIS (IBARA YA 88 (6) (12)): Ni maoni yangu kwamba kiwango kilichopendekezwa cha 75% ya kura za Wabunge kwa ajili ya kuunda Kamati ya Uchunguzi na cha kumwondoa Rais ni cha juu mno. Kwa nini asilimia zaidi ya 50 isitoshe kwa ajili ya kuunda Kamati hiyo na asilimia 66 (theluthi mbili) isitoshe kumwondoa?. Zaidi ya kiwango hicho ni “KULINDANA”.
Pia katiba itamke Rais au kiongozi aliyeondolewa madarakani asistahili kulipwa mafao ya uzeeni – pensheni - kama ilivyo kwa watumishi wengine wa umma wanaofukuzwa kazi..
_ UTARATIBU WA KUBADILISHA KATIBA (IBARA YA 118). Kwa hili tuongozwe pia na uzoefu tuliokwishapata na uzito wa Katiba iliyopitishwa na wananchi. Utararibu wa kubadilisha katiba usiwe rahisi kama huu uliyopendekezwa ambao ndiyo unaotumika sasa. Utaratibu huu ndio ulioiwezesha Chama tawala kwa kutumia wingi wa wabunge wake Bungeni kufuta haki ya raia binafsi kugombea Urais au Ubunge bila ya kuteuliwa na chama cha siasa. Tusiruhusu utaratibu huu wa kubadilisha Katiba uendelee. Napendekeza:
Theluthi mbili wa wabunge kutoka Tanganyika na theluthi mbili kutoka Zanzbar zitahitajika kama ilivyo sasa, na; Theluthi mbili ya wabunge wa upinzani – hawa wanawakilisha wananchi waliowachagua; Kama mabadiliko yanayokusudiwa ni makubwa Ibara 119 iliyopendekezwa naunga mkono.
KUUNDWA KWA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO - UKUBWA WA BUNGE (IBARA YA 113) (na utaratibu wa kuchagua Wabunge): Ibara hii inahitaji uchambuzi wa kina, isije ikashindikana kuitekeleza. Naona Jimbo la uchaguzi eneo lake litakuwa kubwa mno hata kufanya kazi ya wagombea kufanya kampeni kuwa ngumu na yenye gharama kubwa. Yapo pia maswali yakujiuliza: Ilani ya uchaguzi ya chama au mgombea itakuwa na sera za aina gani kuhusu masuala ya Ulinzi na Usalama, Mambo ya Nje nk. ili kuwashawishi wapiga kura wapigiwe kura? Tume ingeangalia uwezekano wa Mabunge ya Nchi Washirika kuchagua wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano kama inavyofanyika sasa kwa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki. Ila Rais atachaguliwa na wananchi. Napendekeza iwe hivyo.
MAJUKUMU YA MKURUGENZI WA UCHAGUZI (IBARA 196 (3)) – Kwamba “Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Uchaguzi atatekeleza majukumu yake kwa kusaidiwa na watendaji ambao ni watumishi wa umma ….”. Mkurugenzi asilazimishwe kutumia watumishi wa umma kama ilivyo sasa. Ushahidi upo unaoonyesha kwamba watumishi hao wanajikuta wanatumikia mabwana wawili- Tume kwa upande mmoja na mwajiri wake kwa upande wa pili ambaye anataka matakwa yake yatekelezwe na hivyo kupotosha haki! Napendekeza Tume iwezeshwe kuajiri/ kuteua watumishi wake ambao watawajibika kwake tu.
11. VYANZO VYA MAPATO YA SERIKALI YA MUUNGANO . (IBARA YA 231) :
1). Pendekezo hili, kwa maoni yangu, litazaa Serikali dhaifu na kuweka Jamhuri ya Muungano kama kivuli. Ni Serikali gani ambayo haina mamlaka ya kutoza kodi wananchi wake ili iweze kuwatumikia ipasavyo? Tunataka Serikali ya Muungano yenye nguvu. Nguvu hii ni pamoja na uwezo wa kupata mapato ya kutosha ya kuendesha Serikali ya Muungano. Mapato hayo yachangiwe na kila mwananchi mwenye uwezo wa kulipa kodi na kila taasisi inayolipa kodi kwa mujibu wa sheria. Kwa utaratibu wa sasa wananchi wanalipa kodi inayoendesha shughuli za Muungano na shughuli za Tanzania Bara na Zanzibar.
Napendekeza pawepo na Chombo cha Muungano kitakachoshirikisha kikamilifu Washirika kitakachosimamia kodi. Pawepo na vigezo vya kugawa kodi inayokusanywa kati ya Serikali ya Muungano na Nchi Washirika. Vigezo hivyo vizingatie ukubwa wa Nchi Mshirika na idadi ya wananchi pamoja na vigezo vingine vinavyoweza kubuniwa na kukubalika. Tunaweza kujifunza kutoka nchi nyingine. Utaratibu huu hautasababisha ongezeko la kodi kwa ajili ya shughuli za Serikali ya Muungano.
Hata kama ushuru wa bidhaa ungetosha (Ibara 231 (a) - hiyo ni kuitenga Serikali na wananchi wake waione kama si yao kwa sababu haigusi mifuko yao. Kwa maoni yangu, Serikali inayoendeshwa na “indirect Tax” na inayolipwa na idadi ndogo ya wananchi ambao wala hawana habari na kodi hiyo, haiwezi kuwa ni Serikali ya wananchi , wala wananchi hawatakuwa na nguvu ya kuihoji Serikali. Kodi yao ndiyo inayowapa nguvu ya kuihoji Serikali.
2). Pendekezo lililotolewa la Nchi Washirika kuchangia -231 (c) - halifai. Itakuwaje na ni hatua gani Serikali ya Muungano itakayochukua kama Mshirika mmoja hachangi kwa sababu mbali mbali? Na ni vigezo gani vitatumika kuchangisha? Kwani hali ya sasa jkoje? Je, wananchi au wawakilishi wao wanajua kama Zanzibar inachangia kiasi gani kwenye bajeti ya kuendesha Mambo ya Muungano? Mapato yapatikane moja kwa moja kutoka vyanzo vyake halisi. Ndiyo kazi itakayofanywa na chombo kilichopendekezwa hapo juu
KUHUSU sifa za kuchaguliwa kuwa mgombea nafasi ya urais au Bunge (ibara ya 79 na. 125), kwa sasa vyama ndivyo vinavyopendekeza- kwa kweli kuteua mgombea. Kumbe baadhi ya walioteuliwa kugombea wasingechaguliwa kama wapiga kura wangewajua. Propoganda za vyama na mashabiki ndizo zinazotawala. Matokeo yake taifa linapata viongozi wabovu na serikali dhaifu.
Napendekeza kwamba pawepo na chombo cha kuchuja na kuhahikiki sifa za wagombea waliopendekezwa na vyama. Kiwe na mamlaka ya kuyakataa na kuagiza vyama vipendekeze wengine au mwingine. Tume ya Uchaguzi ipewe mamlaka hayo. Katika kutekeleza wajibu huu, tume itaongozwa na miiko ya uongozi iliyoorodheshwa katika Katiba hii.
Zipo nchi nyingine zenye utaratibu huo wa kuchuja. Bila kuwa na chombo kama hicho sifa hizo zitabaki kwenye makaratasi na mambo yataendelea kama kawaida tuliyoizoea na taifa litaendelea kupata viongozi wabovu.
Bunge kumshitaki Rais
Ni maoni yangu kwamba kiwango kilichopendekezwa cha asilimia 75 ya kura za wabunge kwa ajili ya kuunda Kamati ya Uchunguzi na cha kumwondoa Rais ni cha juu mno. Kwa nini asilimia zaidi ya 50 isitoshe kwa ajili ya kuunda kamati hiyo na asilimia 66 (theluthi mbili) isitoshe kumwondoaZaidi ya kiwango hicho ni “KULINDANA”.
Pia Katiba itamke Rais au kiongozi aliyeondolewa madarakani asistahili kulipwa mafao ya uzeeni – pensheni - kama ilivyo kwa watumishi wengine wa umma wanaofukuzwa kazi.
Utaratibu wa kubadili Katiba
Kwa hili tuongozwe pia na uzoefu tuliokwishapata na uzito wa Katiba iliyopitishwa na wananchi. Utararibu wa kubadilisha Katiba usiwe rahisi kama huu uliopendekezwa, ambao ndiyo unaotumika sasa. Utaratibu huu ndio uliokiwezesha chama tawala kwa kutumia wingi wa wabunge wake bungeni kufuta haki ya raia binafsi kugombea urais au ubunge bila ya kuteuliwa na chama cha siasa. Tusiruhusu utaratibu huu wa kubadilisha Katiba uendelee.
Napendekeza kwanza, theluthi mbili wa wabunge kutoka Tanganyika na theluthi mbili kutoka Zanzibar zitahitajika kama ilivyo sasa na pili; theluthi mbili ya wabunge wa upinzani – hawa wanawakilisha wananchi waliowachagua, tatu; kama mabadiliko yanayokusudiwa ni makubwa ibara 119 iliyopendekezwa naunga mkono.
Kuundwa kwa Bunge la Jamhuri
Ibara ya 113 inahitaji uchambuzi wa kina, isije ikashindikana kuitekeleza. Naona jimbo la uchaguzi eneo lake litakuwa kubwa mno hata kufanya kazi ya wagombea kufanya kampeni kuwa ngumu na yenye gharama kubwa. Yapo pia maswali ya kujiuliza: Ilani ya uchaguzi ya chama au mgombea itakuwa na sera za aina gani kuhusu masuala ya ulinzi na usalama, mambo ya nje na mengineyo kama hayo ili kuwashawishi wapiga kura wapige kuraTume ingeangalia uwezekano wa mabunge ya nchi washirika kuchagua wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano kama inavyofanyika sasa kwa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki. Ila Rais atachaguliwa na wananchi. Napendekeza iwe hivyo.
Majukumu ya Mkurugenzi wa uchaguzi
Majukumu ya mkurugenzi wa uchaguzi (ibara ya 196; -3) – kwamba “Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Uchaguzi atatekeleza majukumu yake kwa kusaidiwa na watendaji ambao ni watumishi wa umma ….” Mkurugenzi asilazimishwe kutumia watumishi wa umma kama ilivyo sasa. Ushahidi upo unaoonyesha kwamba watumishi hao wanajikuta wanatumikia mabwana wawili- Tume kwa upande mmoja na mwajiri wake kwa upande wa pili ambaye anataka matakwa yake yatekelezwe na hivyo kupotosha haki! Napendekeza Tume iwezeshwe kuajiri au kuteua watumishi wake ambao watawajibika kwake tu.
Vyanzo vya mapato ya serikali ya Muungano
Katika vyanzo vya mapato ya serikali ya Muungano (ibara ya 231) kwanza; pendekezo hili, kwa maoni yangu, litazaa serikali dhaifu na kuweka Jamhuri ya Muungano kama kivuli. Ni serikali gani ambayo haina mamlaka ya kutoza kodi wananchi wake ili iweze kuwatumikia ipasavyo
Tunataka Serikali ya Muungano yenye nguvu. Nguvu hii ni pamoja na uwezo wa kupata mapato ya kutosha ya kuendesha Serikali ya Muungano. Mapato hayo yachangiwe na kila mwananchi mwenye uwezo wa kulipa kodi na kila taasisi inayolipa kodi kwa mujibu wa sheria. Kwa utaratibu wa sasa wananchi wanalipa kodi inayoendesha shughuli za Muungano na shughuli za Tanzania Bara na Zanzibar.
Napendekeza pawepo na Chombo cha Muungano kitakachoshirikisha kikamilifu Washirika kitakachosimamia kodi. Pawepo na vigezo vya kugawa kodi inayokusanywa kati ya Serikali ya Muungano na Nchi Washirika. Vigezo hivyo vizingatie ukubwa wa Nchi Mshirika na idadi ya wananchi pamoja na vigezo vingine vinavyoweza kubuniwa na kukubalika. Tunaweza kujifunza kutoka nchi nyingine. Utaratibu huu hautasababisha ongezeko la kodi kwa ajili ya shughuli za Serikali ya Muungano.
Hata kama ushuru wa bidhaa ungetosha (Ibara 231 (a) - hiyo ni kuitenga Serikali na wananchi wake waione kama si yao kwa sababu haigusi mifuko yao. Kwa maoni yangu, Serikali inayoendeshwa na “indirect Tax” na inayolipwa na idadi ndogo ya wananchi ambao wala hawana habari na kodi hiyo, haiwezi kuwa ni Serikali ya wananchi , wala wananchi hawatakuwa na nguvu ya kuihoji Serikali. Kodi yao ndiyo inayowapa nguvu ya kuihoji Serikali.
Pendekezo lililotolewa la Nchi Washirika kuchangia -231 (c) - halifai. Itakuwaje na ni hatua gani Serikali ya Muungano itakayochukua kama Mshirika mmoja hachangi kwa sababu mbali mbaliNa ni vigezo gani vitatumika kuchangishaKwani hali ya sasa ikojeJe, wananchi au wawakilishi wao wanajua kama Zanzibar inachangia kiasi gani kwenye bajeti ya kuendesha Mambo ya MuunganoMapato yapatikane moja kwa moja kutoka vyanzo vyake halisi. Ndiyo kazi itakayofanywa na chombo kilichopendekezwa hapo juu.
src
Raia mwema