- Madaktari nao walalamikia wenzao
- Nafasi kujiongezea ujuzi zipo, hazitumiki
- Kukiwa na utayari sekta ya afya, India kuikomboa
MIONGONI mwa wagonjwa waliokuwa katika Taasisi ya Saratani ya Hospitali za Apollo katika jiji la Chennai nchini India ni pamoja na daktari kutoka moja ya hospitali za serikali nchini.
Mtaalamu huyo wa afya (jina linahifadhiwa) alijikuta katika mateso yanayomkabili sasa ya saratani kutokana na alichokieleza uzembe wa dhahiri wa wataalamu wenzake, kwamba hawakujali tangu awali alipoanza kusumbuliwa na ugonjwa huo.
Anasema tabia ya uzembe au kutojali ndiyo iliyosababisha kucheleweshwa kubainika kwa tatizo na matibabu yake vile vile. Ni pale aliposhindwa hata kutembea, akawa mtu wa kulazwa ndipo waliposhituka na kumpeleka kwenye hiyo Taasisi jijini Chennai, alipelekwa saratani ikiwa katika kiwango cha juu kabisa.
“Mimi ni daktari mwenzao wamenifanyia hivi, huyo mwananchi wa kawaida hali itakuwaje,” anasema daktari huyo katika maongezo yake na mwandishi wa makala haya, kisha anaongeza:
“Vifaa vilivyotumika kunichunguza hapa hata nyumbani vipo. Ukienda Muhimbili, TMJ na Regency utavikuta. Kwa hiyo vifaa si tatizo. Bali ni akili zetu.”
Inaumiza zaidi unaposikiliza simulizi za mke wake, jinsi walivyohangaika, wakizungushwa na kupewa majibu rahisi, ni mama ambaye, muda wote hivi sasa anautumia pembeni ya kitanda cha mumewe akisali na kumuomba Mungu kumponya mumewe.
Katikati ya majonzi naye hujiuliza, “Huyu ni mwenzao wamemfanyia hivi, hali ikoje kwa wasio wa taaluma hiyo.”
Kauli ya daktari huyo mgonjwa inashabihiana na kauli ya daktari mwingine wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, ambaye anasema madai ya vipato duni na vifaa ni njia ya kutafuta visingizo zaidi katika kukwepa ukweli.
“Lipo tatizo zaidi ya madai ya maslahi na vifaa. Ni tatizo la kitaaluma zaidi, haiwezekani kwa miezi sita mgonjwa alalamikia maumivu ya masaa 24 mfululizo, anaambiwa anasumbuliwa na amoeba. Unampa dawa hakuna nafuu, unaendelea kung’ang’ania amoeba. Hapa tatizo ni taaluma zaidi,” anasema daktari huyo mwanamama.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road, Profesa Twalib Ngoma anaamini kuwa tatizo la msingi katika sekta ya afya nchini ni kuporomoka kwa maadili katika jamii, akibainisha kuwa hakuna sababu ya kumtafuta mchawi katika mazingira ya wazi ya kuporomoka kwa maadili katika jamii.
“Kwani hawa madaktari na wauguzi wanatoka katika jamii ipiSi ni jamii yetu hii hii. Ni rahisi kwa watumishi wa afya kuonekana kwa sababu wanashughulika na binadamu moja kwa moja,” anasema Profesa Ngoma katika mahojiano yake na Raia Mwema jijini Chennai alipotembelea Taasisi hiyo ya Saratani ya Hospitali ya Apollo mwezi uliopita.
Fursa kustawisha fani
Jambo moja linaloshangaza zaidi ndani ya sekta afya nchini ni kwa hospitali za rufaa nchini kutotumia fursa walizopatiwa nchini India kwa ajili ya kustawisha fani zao, fursa ambazo inaaminika zingesaidia hata katika kubadili tabia zisizo za kitaaluma zinazodaiwa kuathiri sekta hiyo.
Katika makubaliano rasmi (MOU) kati ya Serikali ya Tanzania na Hospitali za Apollo nchini India, kipo kipengere cha wataalamu wa afya kutoka Hospitali za Rufaa nchini kwenda nchini India kwa mafunzo katika hospitali ambazo serikali ina mikataba nazo, mpango wa Attachment programs/ exchange programs/ i-service training including post graduates attachments and research for medical and paramedical specialists.
Hata hivyo, taarifa za ndani ya ofisi za Mwambata wa Afya, Ubalozi wa Tanzania nchini India zinabainisha kuwapo idadi ndogo ya wataalamu kutoka Hospitali za Rufaa nchini wanaokwenda India kupitia utaratibu huo.
Umuhimu wa mikataba kuhusu huo utaratibu, ni kutoa fursa kwa wataalamu kutoka hospitali za rufaa nchini kustawisha fani zao pamoja na kujengewa uwezo kupitia mafunzo hayo.
Mfano wa wazi kuhusu umuhimu wa utaratibu huo ni kitengo cha magonjwa ya moyo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambacho baadhi ya wataalamu wake walipata ujuzi wa kibingwa kutoka katika Hospitali hizo na sasa wanafanya upasuaji mkubwa wa moyo (open heart surgeries) kwa weledi mkubwa na wamefanikiwa kupunguza kwa kiasi kikubwa rufaa za wagonjwa wa moyo. Sasa idadi ya wagonjwa wanakuja kwa matibabu ya magonjwa ya moyo nchini India ni asilimia 30 tu.
Hii ni hatua kubwa kwani katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, idadi ya wagonjwa wenye matatizo ya moyo waliokuwa wanapelekwa India ilikuwa zaidi ya asilimia 60 ya wagonjwa wote waliokuwa wanaletwa nchini India kwa matibabu.
Swali linalotatiza baadhi ya viongozi ni kikwazo kiko wapi iwapo serikali imetoa fursa, je, ni wizarani, uongozi wa hospitali zenyewe, au kikundi cha wabinafsi wachache kwenye sekta ya afya?
Kwa upande wake, Mwambata wa Afya katika Ubalozi wa Tanzania nchini India, Dk. Kheri Goloka anabainisha umuhimu wa kuwajengea uwezo watalaamu wa afya katika hospitali za rufaa nchini kwa kuwapeleka India katika kozi fupi fupi ama attachment programs katika hospitali ambazo serikali ina mikataba nazo.
Hospitali ambazo serikali ina makubaliano nazo rasmi ni pamoja na Apollo na Madras Medical Mission.
Pamoja na utaratibu huo, pia anauona umuhimu wa kuendelea kuboresha miundombinu ya hospitali za rufaa nchini, ikiwa ni pamoja na kuzipatia vifaa tiba vya kisasa.
Matibabu ya mtandao (Tele-medicine)
Fursa nyingine isiyotumika na yenye kuibua maswali ni matumizi ya teknolojia ya matibabu ya mtandao ambayo kwa lugha ya Kiingereza hufahamika kama Tele-medicine.
Taarifa za ndani ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii pamoja na Mwambata wa Afya nchini India zinaonyesha kusuasua kwa hospitali za rufaa nchini kuanza kutumia teknolojia hiyo kwa hadi sasa hazijajiunganisha katika mkonga wa Matibabu Mtandao (Tele-Medicines) na hospitali ambazo wizara ina mikataba nazo nchini India.
Mathalani, Mradi wa Matibabu Mtandao (Tele medicine) uliofungwa katika Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) kwa msaada wa Serikali ya India, (katika Mradi wake wa Pan- African e-Network) haujaunganishwa na Hospitali ya Saratani ya Apollo Speciality iliyoko Chennai nchini humo ambayo wagonjwa wenye magonjwa ya saratani wanaopelekwa na Serikali nchini India kutoka ORCI hutibiwa hospitalini hapo.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Seif Rashid anaiangalia huduma hiyo ya matibabu mtandao kama nyenzo muhimu katika kuboresha utoaji huduma za afya nchini akibainisha kuwa ikitumiwa vizuri itaweza kuipunguzia serikali mzigo mkubwa wa kupeleka wagonjwa nje ya nchi kwa matibabu hususani katika kipindi hiki ambapo idadi ya wagonjwa wa saratani wanaopelekwa nchini India inaongezeka kwa kasi.
Kupitia Tele-Medicine Madaktari Bingwa katika hospitali ya ORCI wanaweza kuwasiliana na Madaktari Bingwa wa hospitali za nchini India kupitia on line-medical consultation services pamoja na on line-Continuing Medical Education (CME).
Swali linajirudia tena, tatizo liko wapi, kwani kutokana na hali halisi ya sekta ya afya nchini na nchi nyingi za Bara la Afrika kwa sasa ni taabani, hivyo mtu wa kawaida angetarajia kuona kasi kubwa katika utekeleazaji wake.
Taarifa toka ndani ya wizara hiyo na ofisi ya mwambata wa afya nchini India zinabainisha kuwa tayari Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Marina Njelekela amekuwa akikutana kwa mazungumzo na Rais wa Mtandao wa Matibabu Mtandao wa Hospitali za Apollo nchini India, Profesa Ganapathy Krishnan pamoja na Mwenyekiti wa Hospitali za Apollo za nchini India Dkt. Prathap C. Reddy.
Mikutano ya Dkt. Marina Njelekela imetokana na maandalizi ya serikali, kupitia Ofisi ya Mwambata wa Afya nchini India kumuomba Mwenyekiti wa Hospitali za Apollo Dkt. Prathap C. Reddy, kwa barua ya Mei 24, 201, asaidie kuanzisha huduma ya Matibabu Mtandao (Tele-medicine) katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Mtandao huo utaunganisha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Hospitali za Apollo za nchini India kwa wataalamu nchini kuwasiliana moja kwa moja na wataalamu wenzao wa Hospitali za Apollo za India kwa kubadilishana ujuzi pamoja na kushauriana kuhusu tiba mbalimbali na kutibu wagonjwa wakiwa huku huku nyumbani, Tanzania.
Taarifa zinabainisha kuna makubaliano na kinachoendelea sasa maandalizi ya Mkataba wa Maelewano (MOU) unaopitiwa na pande zote mbili kabla ya kufungwa kwa mtambo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na wataalamu wa huduma hiyo kutoka katika Hospitali ya Apollo Chennai nchini India.
Baadhi ya wataalamu wa sekta ya afya nchini wanabainisha kuwa kufanikiwa kwa mradi huo kutaipunguzia serikali mzigo wa kupeleka wagonjwa nje ya nchi. Wataalamu nchini kupitia Tele-medicine, watawasiliana na wenzao katika Hospitali za Apollo na kushauriana aina gani ya matibabu wapakiwa Tanzania.
Teknolojia hiyo inatumika sehemu mbalimbali duniani kwa sasa ikiwamo India yenyewe, na ni kutokana na ufanisi wake inashauriwa kuharakishwa kwa mradi huo wa Muhimbili ili pia utumike kama mradi wa kuanzia kwa miradi mingine ya Matibabu Mtandao nchini kwa kuunganisha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na hospitali nyingine za rufaa, mikoa na wilaya nchini.
Uhusiano wa Wizara na hospitali hizi za nchini India umezidi kuimarika katika miaka ya hivi karibuni na ushahidi wa hivi karibuni ni hatua ya Serikali kupitia Wizara ya Afya na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kutiliana saini makubaliano ya ujenzi wa hospitali ya kisasa [Modern Multi- Speciality Hospital] pamoja na uanzishwaji wa kliniki za uchunguzi, “Clinics and Dignostics Centres” katika Jiji la Dar es Salaam.
Makubaliano hayo yalisainiwa mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri Mkuu wa India, Dkt. Manmohan Singh alipokuwa nchini Mei 25, 2011.
Eneo la jumla ya hekari 25 limetengwa Kigamboni kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hiyo, wakati ujenzi wa “Clinics and Diagnostics Centres” unaendelea katika jengo la Mwalimu Nyerere Pension Towers, Dar es Salaam na zinatarajiwa kufunguliwa katikati ya mwaka huu 2014.
Kukamilika kwa Mradi huu kutawapunguzia wananchi na serikali mzigo mkubwa wa kupeleka wagonjwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu ambayo ni ya gharama kubwa, na hata kuiwezesha serikali kupiga hatua katika azma yake ya kuifanya Tanzania kitovu cha tiba katika ukanda huu wa Afrika.
Hata hivyo swali linabaki pale pale, nini hasa kikwazo, ni serikali, wataalamu wenyewe, uongozi sekta ya afya au walafi wachache

SRC
Felix Mwakyembe
raia mwema