Monday, March 31, 2014

Mwalimu Mwagane Yeya anayetesa Ligi Kuu

Unapowazungumzia wachezaji wa klabu ya Mbeya City FC wanaofanya vizuri katika Ligi Kuu ya Bara, huwezi kumuacha mshambuliaji Mwagane Yeya.

Kidogo Yeya amepunguzwa kasi katika raundi ya pili ya Ligi Kuu akiwa hajazifumania nyavu hadi sasa. Lakini mshambuliaji huyo alionekana kuwa tishio katika raundi ya kwanza alipopachika mabao sita.

Kati ya mabao hayo, manne alifunga kwa kichwa na mawili alimalizia kwa kiki, sifa zinazomfanya awe mmoja wa wachezaji wachache wanaoweza kutumia vichwa vyao vizuri kuunganisha krosi.

Kwa wale wasiomfahamu vizuri, ni rahisi kwao kuvuta kumbukumbu zao. Alifunga mabao yote vmatatu wakati Mbeya Citu ilipoihenyesha Azam FC kwenye Uwanja wake wa Azam Complex ingawa wenyeji walimudu kusawazisha.

Mshambuliaji huyo alianza kucheza soka akiwa darasa nne katika shule ya msingi Itezi na kushiriki mashindano ya shule za msingi Itezi na kushiriki mashindano ya shule za msingi (UMITASHUMTA) akiwa anacheza nafasi za ulinzi wa kati.
Baada ya kumaliza darasa la saba, Yeya (26) alijiunga na Shule ya Sekondari ya Arage, Mbeya na kujiunga na Black People iliyokuwa ligi daraja la nne. Aliichezea kwa miaka miwili kabla ya kuhamia Uchukuzi ya stendi ya Uyole iliyokuwa ikishiriki ligi daraja la tatu ngazi ya mkoa. Akiwa huko alibadilisha  nafasi na kuwa winga akiwa kidato cha tano na sita kwenye Shule ya Sekondari ya Meta na baadaye kuhamia Kijiweni ya Kigoma.

Alijiunga na Chuo cha Ualimu cha Kasulu na huko aliteuliwa kuchezea kombaini ya mkoa wa Kigoma iliyoshiriki Kombe la Taifa mwaka 2007.

Baada ya kumaliza chuo alijiunga na Zaragoza FC ya Uyole na baadaye kuitwa kombaini ya mkoa wa Mbeya, Mapinduzi Stars mwaka 2008.

Maisha yake Mbeya City FC

Yeya, ambaye ni mwalimu wa masomo ya biashara  wa Shule ya Sekondari Iduda alijiunga na Mbeya City mwaka 2011 baada ya Rhino ya Morogoro kununuliwa na Halmashauri ya Mbeya.


src
mwanachi