Home »
WASANI
» Lady Jaydee, Diamond nani kuvunja rekodi ya 20% KTMA?
- Mzee Yusuph katikati ya Khadija Kopa na Mashauzi
- Muziki wa dansi na vita ya pili kwa ukubwa KTMA 2014
KINYANG’ANYIRO cha Tuzo za Muziki za Kilimanjaro (KTMA 2014), kinaelekea katika hatua ya upigiwaji kura wateule ‘Nominees’, mchakato unaotarajiwa kuanza Aprili Mosi na kuhitimishwa Aprili 30, tayari kwa usiku wa tuzo Mei 3, Mlimani City jijini Dar es Salaam. Kuanza kwa mchakato wa wasanii/vikundi kupigiwa kura, kunatokana na kufungwa rasmi kwa hatua ya kupokea na kuhesabu kura za kupata wateule hao, mchakato uliofanywa na Kampuni ya Auditax International ya jijini Dar es Salaam. Tofauti na miaka iliyotangulia, mchakato wa kupata wateule mwaka huu, uliachwa mikononi mwa wadau wa muziki, ambao walitakiwa kupendekeza wasanii/vikundi wanaoona wanastahili kuingia na kuwania KTMA 2014. Ndiyo kusema washindi wa mwaka huu wa KTMA 2014, watakuwa ni washindi wa wadau na mashabiki, waliotokana na kung’ara kwa kazi zao mwaka 2013. Ushindani unatarajiwa kuwa mkubwa miongoni mwa wasanii vipenzi vya Watanzania.Lady Jaydee, Diamond katika vita ya rekodi KTMAHafla ya kuwatangaza wateule wa kuwania KTMA 2014, uligubikwa na hisia za ushindani kwa wakali wa muziki wa Kizazi Kipya ‘Bongo Flava’ Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ na Nassib Abdul ‘Diamond Platnumz’ wakiwania tuzo saba. Majina ya washindani wa ‘kategori’ 37 za tuzo hizo, yalitangazwa kwenye ukumbi wa mikutano wa Kilimanjaro House, Masaki, ambapo Lady Jaydee ameingia katika kategori saba, ikiwamo moja aliyochaguliwa kutokana na wimbo ‘Kama Huwezi’ alioshirikishwa na Rama Dee. Jaydee ‘Malkia’ na Diamond ‘Mfalme’ wa Bongo Flava, watakuwa na vita kubwa katika vipengele tofauti, iliyotabiriwa na wengi kuweza kuvunja rekodi za mwaka jana katika KTMA, ambapo Omari Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ na Kala Jeremiah walitwaa tuzo tatu kila moja. Anaconda, kama anavyopenda aitwe kwa sasa, atakuwa na mchuano mgumu kutabirika katika kategori nne kati ya saba anazowania tuzo dhidi ya Diamond, ambazo ni Wimbo Bora wa Mwaka, Wimbo Bora wa Afro-Pop, Wimbo Bora wa Kushirikiana na Video Bora ya Muziki ya Mwaka. Vita kuu iko katika Wimbo Bora wa Mwaka, ambapo Jaydee ameingiza nyimbo mbili za ‘Joto Hasira’ na ‘Yahaya’, huku Diamond akiwa na ‘My Number One’ na ‘Muziki Gani’ alioshirikiana na Ney wa Mitego. Katika kategori hiyo, Jaydee na Diamond watapata upinzani kutoka kwa Cassim Mganga anayeiwania kupitia kibao chake ‘I Love You’, pamoja na ‘Kidela’ ya Abdul Kiba ft. Ali Kiba, nyimbo zinazotarajiwa kukoleza upinzani kwa wakali hao. Wakati Jaydee akiwania tuzo ya Wimbo Bora wa Afro-Pop, kupitia ‘Joto Hasira’, Diamond anaiwania na kibao cha ‘My Number One’, nyimbo zitakazochuana na ‘I Love You’ ya Cassim, ‘Kidela’ ya Abdul Kiba ft Ali Kiba, ‘Tupogo’ ya Ommy Dimpoz ft. J. Martins na ‘Roho Yangu’ ya Rich Mavoko. Katika Wimbo Bora wa Kushirikisha/Kushirikiana, ‘Joto Hasira’ wa Jaydee ft. Professa Jay, utachuana na ‘Muziki Gani’ wa Diamond ft. Ney wa Mitego, huku ‘Bila Kukunja Goti’ wa Mwana FA na AY ft J. Martins, ‘Kidela’ wa Abdul Kiba ft. Ali Kiba na ‘Tupogo’ wa Dimpoz ft. J Martins zikiwa kundini. Vita ya mwisho kati ya Jaydee na Diamond, itakuwa katika Video Bora ya Muziki ya Mwaka, ambapo Jaydee ameingia na nyimbo mbili za ‘Joto Hasira’ na ‘Yahaya’, Diamond yuko hapo na ‘My Number One’, zitakazochuana na ‘Uswazi Take Away’ ya Chege ft. Malaika na ‘Mama Yeyo’ ya G Nako ft. Ben Pol. Kategori tatu ambazo Jaydee yu vitani bila Diamond ni Wimbo Bora wa Zouk/Rhumba, ambapo ‘Yahaya’ itakuwa vitani na ‘Yamoto’ wa Mkubwa na Wanawe, ‘Msaliti’ wa Christian Bella, ‘Nakuhitaji’ wa Malaika Band na ‘Narudi Kazini’ wa Beka. Pia Jaydee atakuwa akiwania tuzo ya Wimbo Bora wa R&B kupitia kibao alichoshirikishwa na Rama Dee, kiitwacho ‘Kama Huwezi’, ambacho kitachuana na ‘Listen’ ya Belle 9, ‘Closer’ wa Vanesa Mdee, ‘So Crazy’ wa Maua ft. FA na ‘Wa Ubani’ wa Ben Pol ft. Alice. Katika tuzo ya Mwimbaji Bora wa Kike – Kizazi Kipya, Jaydee atakuwa na ‘vita ndogo’ dhidi ya Vanessa Mdee, Linah na Maua, akitarajia kuwakimbiza ‘wadogo zake hao,’ ingawa inaaminika kuwa hakuna vita rahisi. Kwa upande wake, Diamond atawania tuzo ya Mwimbaji Bora wa Kiume – Kizazi Kipya, anakoumana na Ben Pol, Rich Mavoko, Ommy Dimpoz na Cassim, wakati tuzo ya Mtunzi Bora wa Kiume – Kizazi Kipya atakuwa akipambana na Belle 9, Ben Pol, Rich Mavoko na Rama Dee. Diamond atakuwa vitani na Christian Bella, Abdul Kiba, Ommy Dimpoz na Rich Mavoko katika tuzo ya Mtumbuizaji Bora wa Kiume wa Muziki, tuzo inayokamilisha idadi ya kategori saba ambazo mkali huyo anawania kutwaa tuzo nyingi zaidi ya mwaka jana, ambapo alipata mbili. Hapa ndipo macho na masikio ya wadau na mashabiki yanapokiangalia na kukisikilizia kinyang’anyiro cha KTMA 2014, kujua Je, Lady Jaydee anaweza kuwa mwanamke wa kwanza kutwaa tuzo nyingi? Je, Diamond anaweza kuvunja rekodi ya kutwaa tuzo tano ya Abbas Kinzasa ‘20 Percent’?20 Percent (20%) alinyakulia tuzo tano katika usiku wa tuzo za KTMA 2011, uliofanyika Machi 26, akibebwa na nyimbo zake kadhaa, ikiwamo ‘Money Money’.Maadili yawang’oa Madee, Snura na Jux Akitangaza majina ya wateule, Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), Godfrey Mngereza, alisema mchakato wa kura za wasanii kuingia katika kategori hizo ulikwenda vema, ingawa walilazimika kuziondoa baadhi ya nyimbo zilizopendekezwa kutokana na sababu za kimaadili.“Jumla ya kura 30,000 zilipigwa kupitia ‘sms’ na mitandao, lakini kutokana na sababu za kimaadili, tumelazimika kutupilia mbali mapendekezo yaliyochagua nyimbo za ‘Tema Mate Tuwachape’ wa Madee, ‘Nimevurugwa’ wa Snura na ‘Uzuri Wako’ wa Jux,” alisema Mngereza.Mzee Yusuph katikati ya Khadija Kopa na Isha MashauziMchuano mwingine katika KTMA 2014, uko katika kategori tatu zinazohusisha muziki wa taarabu, ambapo Mfalme Mzee Yusuph yuko katikati ya wanamama mahiri katika aina hiyo ya muziki nchini kwa sasa, Malkia Khadija Kopa ‘Top in Town’ na Isha Ramadhani ‘Isha Mashauzi.’Wakati Kopa na Mashauzi wakitoana jasho katika Tuzo ya Mwimbaji Bora wa Taarab wanakochuana na Khadija Yusuph, Mwanahawa Ali na Leyla Rashid, watakuwa na vita ya aina yake dhidi ya Mzee Yusuph katika Wimbo Bora wa Mwaka wa Taarab. Kopa yuko katika kategori hiyo na kibao chake ‘Fahari ya Mwanamke’, Mashauzi atawania tuzo hiyo na kibao cha ‘Asiyekujua Hakuthamini’ huku Mfalme Yusuph akipambana nao kupitia kibao ‘Wasiwasi Wako’, nyimbo tatu zilizobamba vilivyo mwaka jana. Wakali wengine wanne wanaowania tuzo hiyo na vibao vyao kwenye mabano ni Rahma Machupa (Nipe Stara), Leyla Rashid (Sitaki Shari), Khadija Yusuph (Mambo Bado), na Mwanahawa Ali (Kila Muomba Mungu). Mchuano hapa ‘si wa kitoto.’Nje ya vita hiyo baina ya Mzee Yusuph na kinamama hao, Mfalme atakuwa na vita itayotabiriwa kuwa nyepesi kwake, atakapochuana na Hashimu Saidi na Mohamed Ali ‘Mtoto Pori’ katika kuwania tuzo ya Mwimbaji Bora wa Kiume – Taarab.Muziki wa dansi na vita ya pili kwa ukubwa KTMA 2014Bongo Flava imegubika tuzo hizi, lakini uwapo wa kategori saba zinazohusisha bendi na wasanii wa muziki wa dansi, unamaanisha kuwa aina hiyo ya muziki ina asilimia kubwa ya kuteka hisia za wengi KTMA 2014, licha ya kudorora. Vita kali inayohusisha muziki huo iko katika Tuzo ya Bendi Bora ya Mwaka, ambapo FM Academia, Mapacha Watatu, African Stars ‘Twanga Pepeta’, Akudo Impact, Mashujaa na bendi changa ya Malaika, zitachuana kuwania tuzo inayotetewa na Mashujaa waliyoitwaa mwaka jana. Rapa machachari, Ferguson amepata nafasi ya kutetea tuzo ya Rapa Bora wa Bendi, ambapo yupo pekee miongoni mwa walioiwania mwaka jana. Safari hii akichuana na Kitokololo, Khalid Chokoraa, Canal Top na Totoo ze Bingwa. Mwaka jana aliwashinda Semsekwa, J4, Jonico Flower na Sauti ya Radi. Chaz Baba anatetea tuzo ya Mtunzi Bora wa Mwaka – Bendi, anakochuana tena na Jose Mara, wakiwa vitani na mwanamuziki nyota Christian Bella, Nyoshi El Saadat ‘Mbuyu Usiotingishika’ na Kalala Junior. Ni vita nyingine ngumu kutabiri inayohusisha wakali wa dansi nchini kwa sasa.‘Maprodyuza’ Alan Mapigo, C9, Enrico, Amoroso na Ababuu Mwanazanzibar, watachuana Tuzo ya Mtayarishaji Bora wa Nyimbo wa Mwaka – Bendi, huku Jose Mara, Kalala Junior, Chaz Baba, Khalid Chokoraa na Christian Bela wakiwa katika Tuzo ya Mwimbaji Bora wa Kiume – Bendi. Luiza Mbutu anakabiliwa na upinzani katika kuitetea tuzo ya Mwimbaji Bora wa Kike – Bendi, anakochuana na Catherine ‘Cindy’ na Ciana, wakati vita kuu iko tuzo ya Wimbo Bora wa Mwaka – Bendi, ambapo bendi tano za Kitanzania zinatoana jasho. Bendi hizo na nyimbo zao kwenye mabano ni Mashujaa (Ushamba Mzigo), Victoria Sound (Shamba la Bibi), FM Academia (Chuki ya Nini), Mapacha Watatu (Yarabi Nafsi), na Talent Band (Kiapo Mara 3), zinazotarajiwa kutoana jasho kweli kutokana na kazi zilizowaingiza hapo. Kategori ziko nyingi na wasanii walioingia kuwania tuzo hizo wako wengi. Ndiyo maana waratibu wa tuzo Basata na wadhamini wao Kilimanjaro Premium Lager wakatoa muda kuwawezesha wadau wa sanaa nchini kuwapigia wasanii/vikundi wavipendavyo kura. Kategori nyingine ni: Wimbo Bora Wenye Vionjo vya Asili ya Kitanzania- Kwejaga nyangisha-Batarokota
- Nalonji-Kumpeneka
- Bora Mchawi-Dar Bongo massive
- Tumbo lamsokota-Ashimba
- Aliponji -Wanakijiji
- Agwemwana-Cocodo African music band
Wimbo Bora wa Kiswahili -Bendi- Ushamba mzigo-Mashujaa Band
- Shamba la Bibi -Victoria Sound
- Chuki ya nini -FM Academia
- Yarabi nafsi -Mapacha Watatu
- Kiapo mara 3 -Talent Band
Wimbo Bora wa Reggae - Niwe na wewe-Dabo
- Hakuna Matata-Lonka
- Tell Me-Dj Aron ft Fidempha
- Bado nahitaji-Chikaka ft Bless p & Lazzy B
- Bongo Reggae-Warriors from the east
Wimbo Bora wa Afrika Mashashariki- Tubonge-Jose Chamelleone
- Nakupenda Pia-Waire Ft Allain
- Badilisha-Jose Chamelleone
- Kipepeo-Jaguar
- Kiboko Changu-Aman FT Weizal and Radio
Wimbo Bora wa Taarab - Wasi wasi wako-Mzee Yusuf
- Asiyekujua Hakuthamini-Isha Ramadhani & Saida Ramadhani
- Nipe stara -Rahma Machupa
- Sitaki shari-Leyla Rashid
- Fahari ya Mwanamke-Khadija Kopa
- Mambo bado-Khadija Yusuf
- Kila muomba Mungu -Mwanahawa Ali
Wimbo Bora wa Hip Hop - Bei ya mkaa-Weusi
- Nje ya box-Nick wa pili ft Joh Makini/G-Nako
- Siri ya mchezo-Fid Q ft Nature
- 2030-Roma
- Pesa-Mr Blue Ft Becka Title
Wimbo Bora wa R&B - Listen-Belle 9
- Closer -Vanessa Mdee
- So crazy-Maua ft Fa
- kama huwezi-rama dee ft jay dee
- Wa ubani-Ben Pol ft. Alice
Wimbo Bora wa Ragga/Dancehall - Nishai-Chibwa Ft Juru
- Sex girl-Dr Jahson
- My sweet-Jettyman Dizano
- Feel Alright-Lucky Stone
- Wine-Princess Delyla
Mwimbaji Bora wa Kike – Taarab- Khadija Kopa
- Isha Ramadhani
- Khadija Yusuf
- Mwanahawa Ali
- Leyla Rashid
Mwimbaji Bora wa Kiume – Taarab- Mzee Yusuf
- Hashimu Saidi
- Mohamedi Ali ‘Mtoto Pori’
Mwimbaji Bora wa Kiume – Bendi- Jose Mara
- Kalala Junior
- Chaz Baba
- Khalid Chokoraa
- Christian Bella
Mwimbaji Bora wa Kike – Bendi - Luiza Mbutu
- Catherine ‘Cindy’
- Ciana
Msanii Bora wa - Hip Hop - Fid Q
- Stamina
- Young killer ‘Msodoki’
- Nick wa pili
- G-Nako
Msanii Bora Chipukizi Anayeibukia- Young Killer ‘Msodoki’
- Walter Chilambo
- Y Tony
- Snura
- Meninah
Rapa Bora wa Mwaka – Bendi- Kitokololo
- Khalid Chokoraa
- Ferguson
- Canal Top
- Totoo ze Bingwa
Mtumbuizaji Bora wa Kike wa Muziki - Khadija Kopa
- Vanessa Mdee
- Isha Ramadanni
- Luiza Mbutu
- Catherine ‘Cindy’
Mtayarishaji Bora wa Nyimbo wa Mwaka -Taarab- Enrico
- Ababuu Mwana-Zanzibar
- Bakunde
Mtayarishaji Bora wa Nyimbo wa Mwaka – Kizazi Kipya- Marco chali-Mj Records
- Man Water-Combination Sound
- Mazoo-Mazoo Records
- Sheddy Clever-Burnz Records
- Nahreel -Home Town Record
Mtayarishaji Bora wa Nyimbo wa Mwaka – Bendi- Allan Mapigo
- C9
- Enrico
- Amoroso
- Ababuu Mwana-Zanzibar
Mtunzi Bora wa Mwaka – Taarabu- Mzee Yusuf
- El-Ahad Omary
- El-khatib Rajab
- Kapten Temba
- Sadiki Abdul
- Nassoro Seif
Mtunzi Bora wa Mwaka – Bendi- Christian Bella
- Jose Mara
- Chaz Baba
- Nyoshi El Saadat
- Kalala Junior
Mtunzi Bora wa Mwaka – Hip Hop- Nikki wa Pili
- Young Killer (Msodoki)
- Roma
- Fid Q
- G-Nako
Bendi ya Mwaka - FM Academia
- Mapacha Watatu
- African Stars ‘Twanga Pepeta’
- Akudo Impact
- Malaika Band
- Mashujaa Band
Kikundi cha Mwaka cha Taarab- Jahazi Modern Taarab
- Mashauzi Classic
- Five Stars
Kikundi cha Mwaka cha Kizazi Kipya- Makomandoo
- Navy kenzo
- Weusi
- Mkubwa na Wanawe
src
Tanzania Daima