SHERIA inayokataza vitendo vya kishoga na kusagana iliyopitishwa na Bunge la Uganda na kusainiwa na Rais Yoweri Museveni wan chi hiyo, zaidi ya wiki moja iliyopita imezua mambo.
Kutokana na sheria hiyo, Uganda imejikuta ikiingia katika mgogoro na wafadhili wa nchi za Magharibi ambao wanaamini inakiuka haki za binadamu. Baadhi ya wafadhili tayari wamesitisha misaada kwa nchi hiyo.
Sheria hii si tu inaharamisha mapenzi ya jinsia moja, lakini pia imeweka adhabu kali ambayo ni kifungo cha maisha kwa wahusika na wale watakaoshawishi au kusaidia vitendo hivyo watatumikia kifungo cha miaka saba jela.
Wakati sheria hiyo ikielekea kuharibu uhusiano wa Uganda na wafadhili; mijadala imekuwa ikiendelea barani Afrika hususan miongoni mwa wasomi juu ya nukta mbili zinahohusiana na ushoga.
Nukta ya kwanza ya mjadala ni iwapo mashoga wanazaliwa hivyo au mazingira hususan malezi yanageuza wahusika kuwa mashoga?
Suala hili ambalo linaweza kuamuliwa kwa utafiti wa kisayansi tu limeonekana muhimu kwa sababu watetezi wa ushoga wanadai ushoga unatokana na maumbile ya kibaolojia, hivyo basi kuwaadhibu watu wa ‘jinsi’ hiyo ni kuwaonelea. Watetezi wanaitaka serikali kuwalinda badala ya kuwaadhibu.
Upande mwingine wa mjadala ni wapinga ushoga wanaoamini kuwa kujihusisha na vitendo hivyo hakutokani na maumbile ya kibaolojia bali tabia ya watu wanayojifunza na kuamua binafsi kuishi hivyo. Hawa wanaunga mkono serikali zinazopambana na vitendo hivyo.
Ni bahati mbaya kwamba katika mjadala huu sayansi mpaka sasa imeshindwa kutupa majibu huku utafiti mbalimbali uliowahi kufanyika ukitoa majibu yanayokinzana, yakiunga mkono upande mmoja au mwingine.
Nukta ya pili ya mjadala kuhusu ushoga ni swali kwamba mila na utamaduni wa kiafrika unakataza ushoga? Ni hoja hii inayotumiwa na viongozi wa nchi zetu kupinga ushoga, ikidaiwa ni tabia iliyoletwa na wageni.
Baada ya kufuatilia mjadala huu katika majukwaa mbalimbali ya wasomi, nashawishika kuamini kuwa vitendo hivyo vilikuwapo Afrika na si jambo lililoletwa.
Taarifa moja iliyoitwa ‘Expanded Criminalisation of Homosexuality in Uganda: A flawed Narrative’ iliyoandaliwa na taasisi inayoitwa Sexual Minorities Uganda (SMUG) inataja matukio mbalimbali 21 katika historia ya Afrika yanayothibitisha kuwapo kwa vitendo hivyo Afrika.
Moja kati ya matukio hayo yanahusisha mfalme wa zamani wa Buganda (Kabaka) Daniel Mwanga (1884 -1897), babu Kabaka wa sasa, Ronald Muwenda Mutebi II, ambapo inasemekana alikuwa akifanya mapenzi na raia zake wa wanaume.
Hata hivyo, wanaopinga ushoga kwa hoja za Uafrika wanadai Kabaka Mwanga alifundishwa vitendo hivyo na waarabu, ingawa kwa kuwa yeye ndio mhifadhi wa utamaduni wa jamii yake utetezi huo unaweza usiwe na nguvu, labda kama kuna ushahidi kuwa alichukuliwa hatua za kinidhamu.
Kadhalika katika historia tunajifunza kuwa walioleta sheria dhidi ya vitendo vya ulawiti ni wakoloni wa kiingereza, na sio Waafrika wenyewe. Bado sijakutana na maelezo yanayoonyesha kuwapo kwa jamii ya kiafrika iliyopinga vitendo hivi na kuwaadhibu waliovifanya.
Ukweli wa mambo
Kama wengi wetu tutaamua kuwa wakweli, nina hakika tutakiri kuwa tunapinga vitendo vya mapenzi ya jinsia moja kutokana na mafundisho ya dini zetu, Uislam na Ukristo.
Kwa mujibu wa dini zetu hizi mbili, vitendo hivyo ni haramu na vinachukiza mbele za Mwenyezi Mungu. Katika Uislam kwa mfano, vitendo hivyo viko katika fungu la dhambi kubwa na kwenye nchi zinazotekeleza sheria za kiislamu, adhabu ya kufanya mapenzi ya mwanaume kwa mwanaume ni kifo.
Hata hivyo ni bahati mbaya kuwa baadhi ya viongozi wa dini duniani wameamua kunajisi dini kwa kubariki vitendo hivi wakitumia misahafu hii.
Watetezi wa vitendo vya ushoga wana hoja mbili kubwa moja ikiwepo ya ushoga kuwa ni maumbile na ya pili; ushoga kuwa ni sehemu ya haki za binadamu (ya uhuru wa kuchagua kufanya mapenzi na ampendaye).
Kuhusu ushoga kuwa ni maumbile, ingawa hakuna utafiti uliotoa majibu yanayoweza kumaliza ubishi, swali ambalo watetezi wa ushoga wanapaswa kutusaidia ni je kuzaliwa na ‘walakini’ katika maumbile kunahalalisha kuingiliana watu wa jinsia moja?
Kuhusu hoja ya haki za binadamu, mimi naamini umefika wakati tusione haya kusema tunakataa ushoga kwa sababu ya imani zetu za dini na kwamba madhali sisi ni wengi, demokrasia ichukue mkondo wake kwa matakwa ya wengi kuheshimiwa.
Ni makosa makubwa kwa nchi za magharibi kutarajia dunia nzima iwe kama wao na ndio maana Rais Yoweri Museveni amesema jamii ya Waganda iliyokataa ushoga iachwe ijifunze yenyewe kama imefanya makosa au la maana kama nchi ya Uganda ina haki ya kujitungia sheria zake na ikifika wakati jamii ikaona umuhimu wa kuzibadilisha itafanya hivyo kwa uamuzi huru ya wanajamii.
Ni jambo la kusikitisha kuwa watetezi wa haki za mashoga wanasahau haki za binadamu za walio wengi za uhuru wa kufuata mafundisho ya dini zetu na kufuata maadili ya kifamilia na kijamii. Ushoga kama tabia ‘ambukizi’ unatishia maadili yetu ya kidini.
Kwamba ushoga ni haki za binadamu pia inashangaza na inaelekea mradi wa upanuzi wa maana ya haki za binadamu hautofikia mwisho mpaka kutembea utupu hadharani, mapenzi baina ya ndugu wa damu walioridhiana na hata kujiua zitakapokuwa haki za binadamu.
Cha ajabu ni Waingereza walioleta sheria ya kukataza ulawiti Afrika na leo ndiyo wanaozikana!
Jambo baya zaidi ni kuwa mataifa ya magharibi yanatumia nguvu zao za kiuchumi kutushinikiza kwa kuweka masharti katika misaada. Huku ni kudhalilisha utu na heshima ya Mwafrika, jambo ambalo halipaswi kuvumiliwa.
Pamoja na kuuchukia kwangu ushoga na kuunga mkono nchi zilizotunga sheria za kupambana na vitendo hivyo, mambo matatu, kwa nafasi yetu kama waafrika tunahitaji kuyarekebisha.
Kwanza, wakati tunapanga adhabu kali, jitihada pia zifanyike za kusaidia waliojiingiza katika wa vitendo vya ushoga kujitoa. Nimewahi kusikia kuwa vitendo vya ushoga vina ‘arosto’ (addiction) kama ilivyo kwa wanaotumia dawa za kulevya.
Ingefaa kwa serikali na taasisi zisizo za kiserikali hususan zile za kidini kuanzisha vituo vya kuwashauri na kuwasaidia waathirika. Ni muhimu kuwasaidia waathirika kabla ya kuwahukumu kwa sababu wengine waliingia katika tabia hiyo kutokana na vitendo vya unyanyasaji walivyofanyiwa wakiwa wadogo.
Pili, wazazi katika jamii zetu tujitahidi kuwalinda watoto wetu kwa kutoa uangalizi zaidi kwao na kuchukua hatua za tahadhari. Tusiwalaze watoto wadogo wa kiume na wavulana wakubwa, tukague watoto wetu mara kwa mara, tusilaze wageni au ndugu na watoto na muhimu zaidi tusiwatetee watuhumiwa wa ubakaji, ulawiti ndani ya familia hata kwa kuwawekea dhamana.
Na tatu na mwisho, wale marais waliotuonyesha ushujaa wao katika kupinga ushoga hebu sasa waonyeshe uhodari wao pia katika kupambana na changamoto nyingine muhimu zaidi ambazo nazo huathiri raia wa nchi zao huenda kuliko hata huo ushoga ikiwemo ufisadi, ubakaji na ulawiti wa watoto wadogo na biashara ya dawa za kulevya.
Rais wangu Jakaya Kikwete, hata kama wewe hukuwa na ujasiri wa kuwaambia wazi ‘wakubwa wa dunia’ kuwa na sisi hatuutaki ushoga na tuna sheria inayopinga vitendo hivyo, changamoto nilizozitaja hapo juu zinakuhusu

Kutoka China