Friday, March 14, 2014

BAADHI YA WANAOISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI NJOMBE WAACHA KUTUMIA DAWA KWA KUDANGANYWA NA VIONGOZI WA DINI


 Mwenyekiti  mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania Bi.Fatma Mrisho Akieleza Lengo la Tume Hiyo Kufanya Ziara Ya Siku Mbili Mkoani Njombe.
Na Gabriel  Kilamlya Njombe.

Watu Waishio Na Virusi Vya Ukimwi Katika Mkoa Wa Njombe Wamewatuhumu Baadhi Ya Viongozi Wa Madhehebu Ya Dini Kupotosha Umma Kuwa Wanaponya Ukimwi Kwa Maombi.

Wakizungumza  Mbele Ya Mwenyekiti  Mtendaji Wa   Tume Ya Kudhibiti Ukimwi Tacaids Fatma Mrisho Baadhi Ya Watu Waishio Na Vvu Wamesema Viongozi Wa Dini Wamekuwa Wakiwalagai Waathirika Wa Ukimwi Kuwa Wanaponya Ukimwi Kwa Maombi Na Hivyo Kuacha Kutumia Dawa Na Kupunguza Makali (Arv).

Wamesema Hali Hiyo Imesababisha Baadhi Ya Waathirika  Kuacha Kutumia Dawa Na Kwenda  Kliniki Na Hivyo Kujikuta Katika Hatari Ya Kushambuliwa Zaidi Na Magonjwa Nyemelezi Ya  Ukimwi Na Hivyo Kuhatarisha Maisha Yao.

Wakiwa Kwenye Kikao Cha Wadau Mbalimbali Wa Ukimwi  Wakiwemo Wataalamu Wa Afya Katika Ukumbi Wa Halmashauriya Wilaya Ya Njombe Baadhi Ya

Waathirika Hao Wamesema Viongozi  Hao Wa Dini   Wamekuwa Wakichangia Watu Kuacha Kutumia  Dawa Kwa Kuwadanganya Watu Kuwa Wanaponya Ukimwi Kwa Maombi.

Katika Hatua Nyingine Imegundulika Kuwa Baadhi Ya Waathirika Wamekuwa Wakiacha Kutumia Dawa Hizo Na Badala Yake Wanajiingiza Kwenye  Matumizi Ya Pombe.

Peter  Mwamasika Ni Askofu Mstaafu Wa Kanisa La Kiinjili La Kilutheri  Tanzania Dayosisi Ya Dodoma Na Kamishina Wa Tume Ya Kudhibiti Ukimwi Taifa Kwa Niaba Ya Wakristo Ambaye Amesema Kuwa Pamoja Na Viongozi Wa Dini Kupinga Matumizi Ya Kondomu Lakini Wanapaswa Kuwaelimisha Wananchi Njia Sahihi Za Kutokomeza Janga La Ukimwi.


Tume Hiyo Ilipowasili Katika Shule Ya Msingi Mpechi Ilibaini Kuwepo Kwa Upungufu Mkubwa Wa Walimu Wa Kiume Hali Iliyotajwa Kuwa Inasababisha Kushindwa

Kutolewa Kwa Elimu Ya Ukimwi Kutokana Na Usawa Wa Kijinsi,Ambapo Mmoja Wa Walimu Pekee Wa Kiume Katika Shule Hiyo Alisimama Na Kupaza Sauti Yake Akiomba Serikali Kuongeza Idadi Ya Walimu Wa Kiume Shuleni Hapo.

Kwa Upande  Wake Mwenyekiti Mtendaji Wa Tume Ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania Bi.Fatma Mrisho Amesema Kwa Kuwa Vijana Wamekuwa Wakikumbwa Na Janga La Ukimwi Kuliko Watu Wengine,Serikali Itaendelea Kuhakikisha Vijana Wanaelimishwa Ipasavyo Katika Masuala Ya Kujikinga Na Masuala Ya Ukimwi.

Tume  Hiyo Ya Kudhibiti Ukimwi Imeanza Ziara Ya Kuwatembelea Wananchi Mjini Njombe Kwa Siku Mbili Ambapo Pamoja Na Mambo Mengine Imewafikia Walimu Na Wanafunzi Kwenye Shule Za Msingi Mpechi Na Mount Living Stone Ambapo Hapo Kesho Inahitimisha Ziara Hiyo Ya Siku Mbili Kwa Kutembelea Shule Za Sekondari Ili Kubaini Chanzo Cha Maambukizi Hayo.
 
SRC
EDDY BLOG