Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Ujumbe wake wakiongozana na Balozi wa Tanzania Nchini India John W.H.Kijazi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Indra Gandhi,Rais atakua nchini India kwa ziara rasmi ya siku tisa.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na akizungumza na Balozi wa India nchini Tanzania Debnath Shaw katika ukumbi wa VIP wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Indra Gandhi Nchini India Rais akiwa huko atatembelea sehemu mbali mbali ikiwa ni katika kukuza Uhusiano na mashirikiano ya kiuchumi na Kijamii.