
Vijana wakiwa katika shughuli za kilimo, mkoani Iringa. Picha ya Maktaba.
Kilimo ni sekta inayoajiri zaidi ya asilimia 75 ya Watanzania. Hata hivyo bado ukuaji wake ni wa chini ukilinganisha na sekta nyingine kama vile madini, mawasiliano na uchukuzi.
Wakati uchumi wa Tanzania ukielezwa kukua kwa asilimia saba, sekta ya kilimo inakua kwa asilimia nne tu.
Serikali pamoja na wadau mbalimbali wamekuwa na jitihada za kukuza kilimo, hata hivyo jitihada hizo bado hazijafanikiwa kuinua kilimo na wakulima wenyewe.
Hivi karibuni Jukwaa la Kilimo (Ansaf) na Taasisi ya One ya Afrika Kusini imezindua mwaka wa kilimo wa Afrika unaoandamana na kampeni ya ‘Kilimo Kinalipa, Jikite’, mkoani Iringa ambapo viongozi wa Serikali akiwamo Mkuu wa Mkoa, Dk Christine Ishengoma walishiriki.
Akifafanua kuhusu kampeni hiyo, Katibu Mtendaji wa Ansaf, Audax Rukonge anasema kampeni hiyo ina lengo la kuwataka viongozi wa Afrika kujikita katika mabadiliko ya sera pamoja na uwekezaji kwenye kilimo.
“Kampeni hii ilizinduliwa Januari mwaka huu huko Addis Ababa, Ethiopia katika mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika, kwa dhamira ya kuwahamasisha hasa vijana kuwekeza kwenye kilimo katika kupambana na njaa na kutengeneza ajira na kukuza uchumi,” anasema Rukonge.
Anafafanua, mwaka 2003 viongozi wa Afrika walitia saini Azimio la Maputo na ambalo liliwataka kutenga asilimia 10 ya bajeti zao kwa wizara za kilimo.
Migogoro ya wakulima na wawekezaji inazorotesha uzalishaji, pia inaonyesha umuhimu wa ardhi. Serikali itaendelea kutafuta ufumbuzi wa migogoro yote kwa kusimamia matumizi bora ya ardhi nchini,” anasema.“Hadi sasa ni viongozi wa nchi nane tu, wamefanikiwa kutekeleza agizo hilo huku nyingine 46, Tanzania ikiwamo zimeshindwa kutekeleza.
“Kampeni hii ya One inalenga kuwataka viongozi wa Afrika kutimiza makubaliano hayo kwa kuongeza nguvu katika kilimo cha umwagiliaji, pembejeo, upatikanaji wa masoko, pamoja na haki za wanawake katika umiliki wa ardhi,” anasema Rukonge.
“Umoja wa Afrika umeutangaza mwaka 2014 kuwa mwaka wa kilimo, tutumie fursa hii kupambana na umaskini. Hiyo itawezekana kama kilimo kitapewa kipaumbele,” anasema Rukonge.
Naye mwakilishi wa One, Mercy Erhiawarien anasema changamoto kubwa iliyopo ni kwa nchi za Afrika kushindwa kufikia malengo waliyojiwekea mwaka 2003 ya kutenga asilimia 10 katika bajeti za kilimo.
“Ethiopia, imefanikiwa kupunguza umaskini kwa kupitia kilimo, na huko Ghana uwekezaji katika kilimo umepiga hatua kubwa. Habari kama hiyo pia iko Burkinafaso na inaweza pia kutokea Tanzania,Leo tunataka kuona Tanzania ikikua kiuchumi kwa kukuza kilimo. Hivi karibuni nchi hii imekuwa kiuchumi kwa asilimia 6.6, hata hivyo maendeleo hayo bado hayajaonekana katika kupunguza umaskini. Kilimo ndiyo jawabu la umaskini huu,” amasema Mercy.
Serikali yachechemea
Kaimu Mkurugenzi wa uzalishaji wa mazao katika Wizara ya kilimo, Chakula na Ushirika, Beatus Malema anakiri kuwa bado Serikali haijatimiza Azimio la Maputo hasa kufikisha asilimia 10 ya bajeti ya Wizara ya Kilimo.
“Kilimo ni uti wa mgongo katika kukuza uchumi na kuleta ajira kwa Taifa. Tanzania inajitosheleza kwa chakula kwa kati ya asilimia 112 na 118.
“Hili la kutenga asilimia 10 ya bajeti kwa Wizara ya Kilimo bado halijatekelezwa. Hiyo bado, wakati mwingine tunapanda hadi asilimia tano, sita hadi saba, kwa wastani asilimia tano,” anasema Malema.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk Christine Ishengoma anasema licha ya wakulima kuzalisha chakula kwa Taifa, bado kuna changamoto kubwa.
“Kilimo ni uti wa mgongo wa nchi yetu na kinategemewa hasa na kina mama. Asilimia 75 ya kipato cha Watanzania hutokana na kilimo na husaidia ukuaji wa nchi yetu.
“Hata hivyo wakulima wadogo wana changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na barabara na kukosa maeneo ya uzalishaji na biashara, kukosa masoko ya uhakika, kukosa mikopo ya uhakika na kujitangaza.Kina mama na vijana wana changamoto ya kupata mitaji ya kuendeleza kilimo,” anasema.
Changamoto hizo zinapaswa kutatuliwa na Serikali ili kuwavutia vijana kwa kuwa ndiyo nguvu kazi inayotegemewa.
Anasema Serikali na sekta binafsi wana wajibu wa kuzitatua changamoto hizo ili Tanzania iendelee kuzalisha kwa wingi na kufikia ukuaji wa kilimo kwa asilimia sita kwa mwaka.
“Kuna vijana wapatao milioni moja wanaohitimu masomo yao katika vyuo vyuo mbalimbali. Uwezo wa Serikali wa kuwaajiri watu hao bado ni mdogo. Kilimo ndiyo suluhisho la ajira kwa vijana wetu. Wengine wanaweza kuzalisha shambani wengine wakawa wafanyabiashara na wengine wajasiriamali wa kuongeza thamani ya mazao hayo,” anasema Dk Ishengoma.
Akizungumzia changamoto ya ardhi, Dk Ishengoma anasema matukio ya migogoro ya wakulima na wawekezaji yanazorotesha uzalishaji na uhusiano uliopo.
Migogoro ya wakulima na wawekezaji inazorotesha uzalishaji, pia inaonyesha umuhimu wa ardhi. Serikali itaendelea kutafuta ufumbuzi wa migogoro yote kwa kusimamia matumizi bora ya ardhi nchini,” anasema.
Migogoro ya wakulima na wawekezaji inazorotesha uzalishaji, pia inaonyesha umuhimu wa ardhi. Serikali itaendelea kutafuta ufumbuzi wa migogoro yote kwa kusimamia matumizi bora ya ardhi nchini,” anasema.