
Kichapo! Jamaa wawili wanaotuhumiwa kuwa wezi, nusura wauawe kwa kuchomwa moto na raia wenye hasira kali baada ya kula kichapo ‘hevi’ kwa msala wa kukwapua mkoba wa mrembo aliyekuwa ndani ya Bajaj.
Alisema baada ya kupora mkoba huo walianza kutoka nduki lakini kabla hawajafika mbali, mtu mmoja aliyekuwa na gari, ambaye pia aliona tukio hilo, aliziba njia na kuwafanya vijana hao kutumbukia mtaroni.
rwa, msichana huyo alishuka ndani ya Bajaj na kuanza kuwapigia kelele za wizi hivyo kuwafanya wapita njia kuanza kuwapiga kwa kutumia silaha mbalimbali zikiwemo mawe, fimbo na matofali.
Waandishi wa habari hii waliowahi kufika eneo la tukio, waliwashuhudia watu hao wakipokea kipigo kikali kilichowafanya wawe hoi.
Akizungumzia mazingira ya tukio hilo, Magdalena alisema ana hofu kuwa waliompora, walianza kufuatilia nyendo zake tangu alikotoka nyumbani kwake maeneo ya Mwananyamala, Dar.
“Mimi naweza kusema huu ni mchezo ambao umepangwa tangu naanza safari, kwani wangejuaje kama nimeshikilia mkoba wakati nilikuwa ndani ya Bajaj?” Alihoji msichana huyo ambaye aliomba vijana hao wauawe.
Hata hivyo, wakati jamaa hao wakipokea kipigo kutoka kwa wananchi, baadhi ya watu walipiga simu Kituo cha Polisi cha Kijitonyama ‘Mabatini’, Dar ambao baada ya muda mfupi waliwasili wakiwa tayari kwa lolote.
Lakini katika hali ya kusikitisha zaidi, baada ya vijana hao kupora mkoba huo na kutumbukia mtaroni, baadhi ya watu waliokuwa wakiwapiga, nao waliuchukua mkoba huo na kutoweka nao kusikojulikana.