Wednesday, May 7, 2014

Ripoti ya Twaweza: Je, vituo vya afya vipo kwa ajili ya kuwahudumia watu?

 
Ni mtu 1 tu kati ya watu 20 (6%) mwenye umri zaidi ya miaka 60 na ni mtoto 1 kati ya 5 (18%) mwenye umri chini ya miaka mitano ambao hupata huduma na matibabu bure katika vituo vya afya.

Sera ya Nchi inasema kuwa huduma kwa wagonjwa wa nje kutoka makundi haya mawili ni bure, lakini wananchi wanasema kuwa wanatozwa pesa.

Matokeo haya yametolewa na Twaweza katika muhtasari wa utafiti wenye jina la Je, vituo vya afya vipo kwa ajili ya kuwahudumia watu? Wananchi na watumishi wa afya wazungumzia huduma za afya.

Muhtasari huu ni kwa mujibu wa takwimu kutoka Sauti za Wananchi, utafiti kwa njia ya simu za mkononi, wenye uwakilishi wa kitaifa uliofanyika kwenye kaya zote Tanzania Bara.

Pakua nyaraka