Tuesday, May 20, 2014

Feza Kessy on AyoTV! kaongea kwa dakika 8… South Africa, mpenzi wake, mtoto na mengine ya anakoishi

Screen Shot 2014-05-21 at 6.06.53 AM
Amekua ni sehemu ya Watanzania wanaomiliki headlines nje ya Tanzania lakini ndani ya Afrika baada ya kuiwakilisha nchi kwenye shindano la BIG BROTHER 2013 na kuyaanza mapenzi na staa mwenzake waliekutana BBA Mbotswana O’neal.
Feza ambae anasoma na kuishi Afrika Kusini, aliporudi Dar es salaam siku kadhaa zilizopita alifanya Exclusive interview na AyoTV ambayo alizungumza zaidi ya dakika 25 ila kwa sasa tunakupatia dakika 8 za mwanzo.
Staa huyu ambae ana single mpya ya ‘my papa’ kwenye radio sasa hivi, alivyovizungumzia kwenye hii interview ni pamoja na muziki wake, mtoto wake, mpenzi wake kupata kazi South Afrika baada ya wote wawili kuhamia rasmi nchini humo, jinsi anavyolipwa kwa kutokezea tu kwenye event na ishu nyingine


src
AyoTZ