
Data hizo kwa mara ya kwanza zilionyeshwa kwa ndugu na jamaa za abiria waliokuwa ndani ya ndege ambao wamekuwa wakitaka uwazi zaidi kuhusu taarifa hizo kabla ya data hizo kuwekwa hadharani kwa vyombo vya habari.

Ndege ya MH370 ilipotea Machi 8 mwaka huu wakati ikisafiri kutoka Kuala Lumpur kuelekea Beijing.
Ndani ya ndege hiyo kulikuwa na abiria 239 wengi wakiwa raia wa China ambapo hadi sasa haijapatikana na hakuna sababu maalum iliyotolewa juu ya kupotea kwake