Saturday, April 12, 2014

Zogo lazuka Dodoma, wajumbe waita ripoti ya Kamati No. 1 ‘maoni binafsi’ [VIDEO]


SHARE THIS STORY
 
   Dodoma. Zogo kubwa limezuka Bunge Maalum la Katiba wakati wa uwasilishaji wa taarifa za kamati baada ya mmoja wa wenyeviti wa kamati hizo kudaiwa kukiuka kanuni.
Mwenyekiti wa Kamati Na. 1, Ummy Mwalimu, ametuhumiwa kukiuka kanuni kutokana na kutokusoma ripoti iliyoainisha maoni ya timu yake kama ilivyoandikwa.
Wajumbe walidai kuwa Mh. Mwalimu ametoa maoni yake binafsi ambayo hayapo kwenye taarifa ya kamati.
Pamoja na jitihada za Makamu Mwenyekiti wa Bunge hilo Maalum la Katiba, Samia Suluhu Hassan, kupoza rabsha hizo, Mh. Mwalimu alizidi kuzua zogo pale aliporuka baadhi ya mapendekezo ya Walio Wachache katika ripoti yake

src
mwananchi