Saturday, April 5, 2014

Z Anto: Kifo cha mama kimenipoteza


Z Anto: Kifo cha mama kimenipoteza


BAADA ya kuwa kimya kwa muda mrefu, Ally Mohamed ‘Z Anto’ amesema ukimya wake umesababishwa na kufiwa na mama yake mzazi aliyefariki dunia Julai, mwaka jana.
Z  Anto ni miongoni mwa wasanii ambao walifanya vizuri miaka ya nyuma kutokana na ubora wa kazi zake ambazo zilikuwa na mvuto kwa jamii inayomzunguka.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Z Anto alisema aliamua kuwa kimya kwa lengo la kumkumbuka mama yake, kwa sababu alimpenda sana na hakutarajia kama atampoteza kwa kipindi hicho.
“Nililazimika sana kukaa kimya kwa sababu ya kumpoteza bi mkubwa, mara nyingi nikienda katika shoo zangu nilikuwa namletea zawadi, alivyoondoka sikuona sababu ya kuendelea kufanya muziki wakati nina uchungu,” alisema.
Msanii huyo kwa sasa anatamba na kibao chake kinachojulikana kwa jina la ‘Ukipendwa Ringa’, ambao umeanza kufanya vizuri kutokana na ubora wa mashairi yaliyosimama ndani yake.
Z Anto alishawahi kutamba na kazi zake kama, Binti Kiziwi, Kisiwa cha Malavidavi, Mpenzi Jini na nyinginezo nyingi

src
Tanzania Daima