Thursday, April 10, 2014

KUMBE HII SIYO BONGO TU:TAZAMA VIDEO 5 ZILIZOPIGWA MARUFUKU KUCHEZWA RWANDA

Screen Shot 2014-04-10 at 11.02.44 AM

Labda tunaweza kudhani ni Tanzania tu ndio imeingia kwenye headlines za kufungia video za nyimbo kadhaa za Wasanii ila ukweli ni kwamba hata kwenye nchi zinazoizunguka Tz kama Uganda, Rwanda na Kenya zimefanya hivyo.
Post hii ni maalum kwa ajili ya stori kutoka Rwanda kuhusu video hizi tatu ambazo haziruhusiwi kuchezwa kwenye vituo vya TV kwa sababu zimevunja maadili ambapo Wizara ya Utamaduni iliitisha mkutano na Waandishi wa habari na kusema iko tayari kulipia gharama za video kurudiwa lakini ziwe na maadili, yani bila picha za uchi au za kimahaba zinazoonekana.
Rafiki yangu TK ambae ni mtangazaji wa TV Rwanda ananiambia Rais Paul Kagame alishawahi kusema kwenye moja ya hotuba zake kwamba pamoja na nyimbo kufungiwa, >>> ‘kufungia nyimbo za Wasanii kisa wamekiuka maadili sio dawa, tatizo ni walifundishwa maadili wakakiuka? kuwafungia sio dawa ya kuwafundisha utamaduni… kuna njia nyingine za kuwasaidia’


Hii ya kwanza hapa juu ni ya Urban boyz inaitwa ‘ancilla’

src
AyoTZ