
millardayo.com imekutana na mbunge wa Kawe Mh. Halima Mdee ambae hili ni eneo lake na anasema ‘Manispaa yetu ya Kinondoni kuanzia mwaka 1995, 2000 na 2005 watu walifanya kama ni shamba la bibi, kila mtu alikua anachuma anachotaka pasipo kujali mipango miji ikoje ama sheria zinasema nini’

‘Sasa Wachakachuzi wa viwanja enzi hizo wakauza haya maeneo na watu wakajenga majengo yao yakaziba mifereji ambayo ilikua imetengenezwa kwa makusudi ya kupeleka maji baharini sasa mvua zikinyesha maji yanajaa, sasa maskini kuna Wananchi wangu wa bonde la mpunga kule yani ndio wanaathirika zaidi pamoja na wapita njia hivyo ikabidi tutafute pesa kupitia mfuko wa barabara na sasa kazi inaendelea’

‘Bilioni sita hii itatumika kujenga mifereji mikubwa ambayo itaanzia pale Mikocheni A darajani mpaka huku TANESCO alafu itashuka kuelekea baharini na itasaidia sana Wananchi wangu wa bonde la Mpunga ambao wanateseka sana, inajengwa lami kwa mara ya kwanza barabara ya Maandazi (Maandazi road)’

Hii mvua ikiisha na zile project zikiendelea vizuri hiyo miaka ya mbele inayokuja itakwenda vizuri lakini zaidi wote ambao wanatumia barabara ya Bagamoyo ya zamani kwenda Mikocheni, Mabwepande, Kawe na wengine wanaopata mafuriko, kwa ukubwa wa makaravati niliouona naamini itapunguza kero hii kwa muda mrefu, project ya mifereji haitakiwi kuchukua miezi sita ila hii mvua imevuruga mambo mengi sana’
src
millard Ayo